Aliyekuwa Rais wa Wapalestina Hayati Yasser Arafat |
Rais wa PLO, chama kilichokuwa
kikipigania Uhuru wa Taifa la Wapalestina, imebainika ya kwamba huenda alikufa
kutokana na kuwekewa sumu hatari ijulikanayo kama Polonium 210. Wataalamu kutoka
nchi ya Uswisi ndio waliofanya uchunguzi huo baada ya uchunguzi wa awali
kubaini kiasi kikubwa cha kemikali hiyo katika sampuli za mabaki ya mwili wake.
Mjane wa Arafat, na mumewe enzi za uhai wake |
Mjane wa Marehemu Suha na mwanawe
Zahwa wameapa kuchukua hatua zote kuhakikisha haki inapatikana. Kifo cha Yasser
Arafat kilitokea mnamo mwezi November mwaka 2004 baada ya kuugua homa kali
isiyojulikana akiwa mjini Ramallah. Wapalestina wanaituhumu Israel kuhusika
lakini Taifa hilo linakanusha vikali.
DW
0 Response to "RAISI WA PALESTINA YASSER ARAFAT ALIUWAWA KWA SUMU HATARI YA POLONIUM"
Post a Comment