Kile chombo kilichorushwa na
Idara ya mambo ya Anga za juu ya India hivi karibuni kwenda Sayari nyekundu ya Mars
kimekwaa kisiki baada ya injini yake
kufeli kukirusha chombo hicho kutoka katika tabaka la nguvu za uvutano la
dunia.
Tatizo hilo lilitokea
marekebisho yalipokuwa yakifanywa ili kukiongezea nguvu ili kiweze kufikia kasi
yake ya juu kutoka Km.71,623 hadi Km.100,000 ili kuweza kufikia umbali wake wa
juu. Hata hivyo Mkuu wa shirika la utafiti wa anga alisema chombo hicho bado
kingali dhabiti.
Kutokana na tatizo hilo,
chombo hicho sasa hakitaruka tena moja kwa moja kuelekea Sayari ya Mars na
badala yake itabidi kiendelee kuizunguka Dunia mpaka pale matengenezo muhimu
yatakapofanywa ili kiwe na uwezo wa kulivuka tabaka la nguvu za uvutano la
Dunia kuelekea anga za juu zaidi zilipo sayari nyinginezo ikiwemo na hii ya
Mars.
Ikiwa nchi ya India itafaulu
katika jaribio lake hili, itakuwa ni Taifa la nne baada ya Marekani, Urusi na
Jumuiya ya Ulaya kurusha chombo kwenda katika Sayari hii ya Mars.
0 Response to "SAFARI YA INDIA KWENDA SAYARI YA MARS YAKWAA KISIKI"
Post a Comment