Wachunguzi WA Umoja wa Mataifa nchini DRC ambao
walifanya uchunguzi katika maeneo yaliyokimbiwa na waliokuwa waasi wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kwamba wameshangazwa sana na idadi kubwa ya
silaha walizoacha M23 baada ya kukimbia na kuziacha uwanja wa mapambano na
kwamba ni lazima walikuwa wakipata ufadhili wa hali ya juu kutoka mahali
fulani.
Wakati huo huo, Uganda
imesema kuwa haitawakabidhi kwa serikali ya
Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo waasi
wa kundi la M23 ambao wamekimbilia nchini
humo baada ya kushindwa na majeshi ya
Kongo. Msemaji wa jeshi na wizara ya
ulinzi, kanali Paddy Ankunda, ameliambia shirika la
habari la AFP kuwa waasi hao si
wafungwa, ni wanajeshi ambao wanakimbia vita
na kwa hiyo Uganda inawapokea na kuwasaidia
kwa sababu ni wajibu wa nchi hiyo.
Ameongeza kuwa
Uganda pia imewakaribisha wanajeshi waliokimbia
kutoka katika jeshi la Jamhuri ya
kidemokrasi ya Kongo mapema mwaka huu. Kundi la M23
lililoundwa miezi 18 iliyopita, ambalo Rwanda na
Uganda zinashutumiwa kwa kuliunga mkono, lilishindwa
na jeshi la Kongo ambalo limekuwa
likisaidiwa na majeshi ya Umoja wa
Mataifa siku ya Jumanne na kutangaza kuwa
limesitisha operesheni zake za kijeshi. Jeshi la
Uganda limesema jana kuwa kiasi ya wapiganaji
1,500 wa M23 wamevuka mpaka na kujisalimisha
nchini humo.
0 Response to "SILAHA WALIZOACHA M23 NI ZA KUTISHA"
Post a Comment