1. Utangulizi
Katika kikao chake cha
siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA,
pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani
ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi
wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za
kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama
kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba
waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama
ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu.
Sababu za kufukuzwa
kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo
si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama.
Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa
kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama
ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.
Ninatambua kwamba chama
changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana
kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki
ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki
mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie
CHADEMA. Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho
kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho.
2. Kuhusu tuhuma
mbalimbali zinazo elekezwa kwangu
Zipo tuhuma nyingi
ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na
baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni
mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha
tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao
mbalimbali vya chama.
i) Tuhuma kwamba
sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka
2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:
Mimi nilikuwa mgombea wa
ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge,
nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo
Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote
wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea
urais.Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na
Rais.Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za
Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.
ii) Tuhuma kwamba katika
Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke
yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana
kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua.
iii) Tuhuma kwamba
nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika
uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa
njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na
Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama
jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa
ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama
na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama
kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi
wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho.
iv) Tuhuma kwamba
nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba
nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi.
Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012
baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012
kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi.
Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi
kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko.
v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha
chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba
mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama
'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na
kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika
taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa
na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:
Utawala bora hautaki
mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea
vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga
na ambazo tunapigania kuzibadilishaNapenda kusisitiza kwamba hakuna chama
ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa
nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu
ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila
kujali kosa hili ni la nani.
vi) Tuhuma kwamba mimi
ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao
Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

Sipokei posho yeyote ya
vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja
na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye
ushahidi vinginevyo auweke hadharani.Swala la kukataa posho (sitting allowance)
ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi.
Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake
100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya
bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza
matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari
wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa
vifo vingi vya kina mama.Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na
Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.
3. Usambazaji wa Ripoti
ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:

Kwamba baadhi ya
waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati
mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu.
Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu
za chama chetu.Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu,
nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika
kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
4. Hitimisho
Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.

Naomba wanachama waelewe
kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa
na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu,
ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama
chetu.
Kama mwanasiasa kijana
niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna
maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya
siasa.
Kinachoendelea ndani ya
chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda
demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na
wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa
ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima
upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu,
'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana
kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013
chanzo Mjengwablog
0 Response to "TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA"
Post a Comment