Hifadhi ya Katavi, picha na tovuti ya tazamaramanitanzania.com |
MKUU wa
Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima, amewataka vijana wilayani
Mpanda kujiajiri kuliko kupoteza muda kushinda vijiweni.
Alisema serikali katika bajeti ya mwaka huu ilitenga sh bilioni
moja kwa ajili ya mikopo ya vijana, lakini cha kushangaza badala ya vijana
kuunda vikundi ili wanufaike na mikopo, kila kijana anataka kununua pikipiki.
Alisema ni vizuri wazee wakawashauri vijana wao wakafanya
shughuli za miradi za muda mrefu ambazo zinaendana na wakati na
zitakazoleta faida na tija kwa jamii.
Aidha aliwataka wazee wa Mpanda kutoutumia umoja wao huo
kwa misingi ya ukabila wala dini, kwani wakiendesha umoja huo kwa misingi
hiyo watafanya kukosa upendo miongoni mwao.
Alisema watu wanaamini wazee ndiye kimbilio la vijana,
hivyo hawapaswi kuwa na mfarakano wa aina yoyote.
Pamoja na hayo, umoja huo umeeleza changamoto wanazokabiliana
nazo kuwa ni matatizo ya uongozi, katiba na matatizo ya fedha.
Mmoja wa wazee hao, Kassim Mfaume, alieleza katiba yao ina
kasoro mbalimbai ambapo endapo hazitarekebishwa zinaweza kuleta athari
baadaye.
HABARI NA: Tanzania Daima.
0 Response to "VIJANA MPANDA WATAKIWA KUJIAJIRI"
Post a Comment