WAHITIMU
wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kuhakikisha elimu waliyoipata
inabadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Wito huo ulitolewa juzi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga, Bernard Maselina, kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Eckenford mkoani hapa.
Alisema wahitumu hao wanapaswa kuhakikisha elimu waliyoipata
inawasaidia kutatua mambo ya msingi na kuwa chachu ya mabadiliko katika vijiji
vyao, mkoa na taifa kwa ujumla.
“Tunajua ugumu wa shule, hongereni kwa kumaliza.
Mkakitangaze vema chuo hiki kwani sitarajii kumuona mhitimu akizurura mitaani,”
alisema Katibu Tawala.
Mmiliki wa chuo taasisi ya Eckenford, Remens Tarimo, aliwaasa
wahitimu hao kuitumia vema elimu hiyo na kuhakikisha inakuwa mkombozi wa maisha
yao kwa kuwa wabunifu katika kila nyanja.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu hao, Agness Mushi, alisema
wanaahidi kuwa wazalendo na waadilifu katika kuitumikia nchi kwa kupitia
elimu waliyoipata na kuahidi kuwa watakitangaza vema chuo hicho.
Jumla ya wahitimu 327 katika ngazi ya shahada, Stashahada na
Astashahada wamehitimu katika chuo hicho.
CHANZO: Tanzania Daima.
0 Response to "WAHITIMU WATAKIWA KUWA WABUNIFU"
Post a Comment