Asema kijana ndiye Aliyeanza
kumtongoza.
Hatimaye Mbunge Rosweeter
Kasikila (60), aliyefunga ndoa na kijana mwenye umri wa miaka 26, amefunguka
kwa kusema aliyeng'ang'ania kufunga ndoa hiyo ni kijana mwenyewe licha ya
kumtahadharisha tofauti ya umri wao.
Kasikila alitoa kauli
hiyo jana, baada ya kutakiwa kujibu shutuma zilizotolewa na mumewe huyo,
Michael Christian (26) ya kung'ang’ania vyeti vyake vya elimu kwa lengo la
kumtaka arudi nyumbani.
Christian aliyefika
katika ofisi za NIPASHE jana alitoa nakala ya barua aliyoituma kwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuomba atumie uwezo wake wa
kisheria ili mbunge huyo amrudishie vyeti vyake alinavyovishikilia.
Kufuatia maelezo hayo, NIPASHE ilimtafuta Dk. Nchimbi kwa njia ya simu ili athibitishe kupokea nakala ya barua hiyo lakini simu yake ilikuwa imezimwa.
Nakala nyingine za
barua hiyo zilitumwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu
kwa jamii-Madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga, Mchungaji wa
Kanisa la Assembilies of God, Mikocheni B, Mchungaji Getrude Rwakatare na
vyombo vya habari.
Akijibu shutuma hizo,
mbunge huyo alisema hajawahi kung'ang'ania vyeti vya kijana huyo wala
kulazimisha ndoa kama anavyodai Christian.
"Nahisi kuna watu
wanamtumia ili wanichafue, siwezi kung'ang'ania vyeti, kwanza vya kazi gani
kwangu, ukweli ni kwamba Michael, shida yake anataka nichafuliwe, kwangu
aliondoka wakati sipo, sasa hivyo vyeti nimeving'ang'ania saa ngapi,"
alisema na kuongeza:
"Mwaka jana
nikiwa Dodoma nilipata taarifa ameondoka nyumbani, kweli nilivyorudi nilikuta
amechukua vitu vyake vyote kasoro tu vile nilivyomnunulia, hivyo vyeti
anavyosema nimeving'ang'ania mbona hajawahi kutamka mbele yangu zaidi nimeona
kwenye magazeti," alihoji.
Alisema baada ya
kufika nyumbani alipata taarifa kuwa, mume wake huyo amepanga chumba na anaishi
na mwanamke mwingine (askari) ambaye ni mjamzito.
Alisema utaratibu
alioutumia kijana huyo wa kumchafua kwenye magazeti siyo sahihi na kumshauri
angeenda mahakamani au kanisani kama aliona haitaki ndoa tena.
Aliongeza kuwa yeye na
Christian walifahamiana mwaka 2009 baada ya kufiwa na mume wake aliyemtaja kwa
jina moja la Mushi.
"Sikumtongoza
kama anavyosema, alikuja katika hospitali ya Bagamoyo akitokea chuo cha Red
Cross wakati huo nilikuwa Muuguzi Mkuu, aliponiona alinipenda alianza
kunitongoza, nilimkatalia na kumwambia mimi ni mtu mzima sana kwake, "
alisema na kuongeza:
"Alikuwa
ananitumia email (barua pepe) za kunitaka, nilimwambia umri wangu ni mkubwa,
lakini yeye alikuwa ananiambia kwenye vitabu vya dini kuna sehemu gani
kumeandikwa umri," alisema.
Alisema alijikuta
ametumbukia kwenye penzi la kijana huyo na kuanza mahusiano naye.
"Nina nakala zote
za vidhibitisho ambavyo alikuwa akinitumia kunitongoza nimevichapisha kama
vielelezo vyangu, tena wakati tumeanza uhusiano Taasisi ya Safina ambayo
ilikuwa ikimsaidia katika masomo yake, ilinipigia simu," alisema na
kuongeza:
"Safina walitaka
kujua kama nina mahusiano na huyu kijana niliwajibu ni kweli, waliniambia kama
ndiyo hivyo wanafuta kumsaidia kwa sababu wao huwasaidia wale ambao hawana uwezo,
yatima, " alisema.
Kijana Michael Christian (26) |
Alisema wakati taasisi
hiyo ikimfuta, ilikuwa imemlipia Christian sehemu ya ada ya masomo aliyokuwa
akiyachukua."
"Nililazimika
kumlipia ada ya mwaka wa pili na watatu wa masomo yake pamoja na mambo mengine
na ilifika kipindi aliniambia anataka kunioa, ndipo tulipofanya mchakato ambapo
nilitolewa mahari na ndoa ilifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutangazwa
mara tatu," alisema.
Alisema Christian
alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa mahari ya Sh. 200,000 na baada
ya harusi alipelekwa Kondoa kwa ndugu wa kijana huyo.
"Huko tulienda
kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka jana, tulifanyiwa sherehe za kimila na
ndugu za mume wangu ambao ni baba mdogo, bibi mzaa baba yake na shangazi, pia
ndugu zake wa Kimara na Dodoma wananijua, " alisema.
Hata hivyo, mbunge
huyo alipoulizwa kama ndoa hiyo ipo sasa hasa kufuatia shutuma hizo, alisema
hawezi kujua kwa sababu mume wake aliondoka bila kumuaga na kwa sasa anaishi na
mwanamke mwingine toka Novemba mwaka jana.
Alisema wakati wa
mahusiano yao wafanyakazi wenzake Christian walikuwa wakimhoji kwa nini ameamua
kuwa na mtu mzima kama (mbunge), lakini yeye aliwajibu hakuna umri kwenye
biblia.
Alipoulizwa kama ana
mpango wa kuchukua hatua dhidi ya kijana huyo, mbunge huyo alisema hana mpango.
Mbunge huyo alijitetea kuwa, hakumlazimisha
kufunga ndoa na kwamba wakati kijana huyo akimtongoza, alimweleza kuwa hawezi
kuzaa kwa sababu umri wake umeshapita.
0 Response to "YULE MBUNGE MWANAMAMA MIAKA 60 ALIYEOLEWA NA KIJANA UMRI WA WANAWE HATIMAYE AFUNGUKA"
Post a Comment