Viongozi Wakuu wa Chadema |
Chama
Cha Kidemokrasia na Maendeleo CHADEMA leo hii kimewavua uongozi viongozi watatu
wa chama hicho kwa makosa ya kugundulika waraka unaodaiwa ni wa
kukisambaratisha chama vipande vipande na unaowashutumu mwenyekiti wa
chama Freeman Mbowe pamoja viongozi
wengine waandamizi wa Chama hicho.
Wanachama hao waliovuliwa uongozi ni, aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu Bwana Zitto Kabwe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoani wa Arusha,Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu Dr.Kitila Mkumbo.
Mwanasheria wa CHADEMA Mheshimiwa Tundu Lissu |
Maamuzi
hayo yamechukuliwa na Kamati Kuu ya chama katika kikao cha siku mbili
kilichofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam. Mwanasheria wa
chama hicho Mheshimiwa Tundu Lissu akizungumza alidai kwamba katika waraka huo
alitajwa mtu kwa jina MM ambaye
ndiyo Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni
Mwigamba na M2 bado hakujulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chama.
Waraka huo uliopewa jina la la Waraka wa ushindi umedaiwa na Mheshimiwa Lissu kwamba unavunja katiba ya Chama kwa sababu
umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na
katiba ya CHADEMA. Ameendelea kusema kwamba tuhuma zote zilizoko katika waraka
huo hazijawahi kuwasilishwa rasmi katika kikao chochote halali cha chama,
kinyume na matakwa na masharti ya katiba ya chama cha CHADEMA.
0 Response to "ZITTO KABWE, DR. KITILA MKUMBO PAMOJA NA SAMSON MWIGAMBA WATIMULIWA UONGOZI CHADEMA"
Post a Comment