Ndugu zangu,
Kuna habari kubwa leo;
mkutano wa Zitto na Dr. Kitila Mkumbo na Watangazaji wa habari.
Wengine sisi ni wadadisi
na wachambuzi wa habari. Kuna wanaotuita wachunguzi wa mambo. Na ndio kazi
ninayoifanya sasa.
Naam, nimesoma ya magazetini na michango ya mitandaoni kuhusiana na sakata la Zitto na chama chake, Chadema.
Nionavyo, Chadema kwa sasa
iko kwenye ' Civil War'- Ni vita yake ya ndani, lakini, kuna walio nje ya
Chadema wanayoifuatilia kwa karibu sana vita hii, ikiwemo ' Watani' wao wa
jadi, CCM.
Na CCM hawana hata kimoja cha kuiombea heri Chadema kwenye vita
hii ya ndani ya chama hicho. Anayefikiri vingine hazijui siasa za nchi hii.
Kuna mawili yanayoweza
kutokea kwenye ' Civil War' hii ya Chadema; Mosi, kuwa yaweza kuwa mwanzo wa
mwisho wa Chadema au mwanzo wa mwisho wa Zitto Kabwe. Ni mwanzo wa mwisho wa
Chadema kama chama kikuu cha upinzani. Ni mwanzo wa mwisho wa Zitto kama
kiongozi anayeshimika na makini kwenye siasa za upinzani na harakati za kuleta
mabadiliko ya kimsingi nchini. Hii ni vita isiyo
na matokeo ya kutoka sare, lazima mshindi apatikane.(P.T)
0 Response to "ZITTO NA ANACHOKWENDA KUSEMA KWA WATANGAZAJI WA HABARI...!"
Post a Comment