Waziri wa habari nchini humo Lambert Mende kwa sasa hali
imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa
wakiendesha mashambulizi hayo.
Watu hao waliokuwa na
silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16
wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya
Taifa.
Amesema kuwa kulikuwa na
mtukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi
ya jeshi.
Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao waliokuwa wakiendesha
mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa
walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya
kusababisha madhara .
Mashambulizi haya
yametokea wakati rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga
nchini humo.
Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhali kwa raia wake kutofanya
safari za ndani ya mji wa Kinsasa hadi hali itakapodhibitiwa Zaidi.
CHANZO BBC SWAHILI
0 Response to "HATIMAYE JESHI LA KONGO LAREJESHA HALI YA UTULIVU MJINI KINSHASA"
Post a Comment