MELI KUBWA YA UTAFITI YA KIRUSI YAKWAMA KWENYE BARAFU BAHARINI IKIWA NA WANASAYANSI 74 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MELI KUBWA YA UTAFITI YA KIRUSI YAKWAMA KWENYE BARAFU BAHARINI IKIWA NA WANASAYANSI 74

Meli ya Australia imo njiani kuelekea Mashariki wa Antarctica kwa ajili ya kukwamua meli ya wanasayansi iliyokwama kwenye theluji tangu siku ya jumanne.

Awali juhudi za uokoaji zilifanywa na wavuja theluji wa Uchina na Ufaransa lakini walikwama kutokana na unene wa theluji.

Hata hivyo mwandishi wa habari wa BBC aliyepo kwenye meli ya utafiti ya Urusi anasema tayari theluji imeanza kupasuka na kuongeza matumaini ya meli hiyo iliyonasa kujikwamua yenyewe na kuanza kuondoka.

Wanasayansi wapatao sabini na nne, watalii na wafanyakazi wa meli wapo kwenye meli hiyo iliyokwama inayoitwa .
Meli hiyo imekuwa ikitumiwa na taasisi ya Australasian Antarctic Expedition kufuatilia njia mtafiti Douglas Mawson aliyesafiri kwenye njia hiyo karne iliyopita.

Shokalskiy imejaa chakula cha kutosha na hakuna hatari hii ni kwa mujibu wa timu ya uokoaji.
Pamoja na kunasa, wanasayansi wanaendelea na majaribio ya kisayansi, kupima nyuzi joto kuzunguka theluji iliyoanza kupasuka.

Mamlaka ya Usalama wa Majini ya Australia ambayo ndio inayoratibu uokoaji imesema kikosi cha uokoaji cha Aurora Australis kilitarajiwa kuwasili katika eneo meli hiyo iliponasa siku ya jumapili majira ya saa 9 kwa saa za Afrika Mashariki.

Mitambo mikubwa ya kukata theluji ina uwezo wa kukata theluji yenye unene wa mita 1.6 na uwezo wa kuzoa theluji ya ukuta wa mita tatu kuzunguka eneo la Shokalskiy.

Kama operesheni hiyo ya uokaji itashindikana itabidi helkopa zitumike kuwaokoa.

CHANZO: BBC

0 Response to "MELI KUBWA YA UTAFITI YA KIRUSI YAKWAMA KWENYE BARAFU BAHARINI IKIWA NA WANASAYANSI 74"

Post a Comment