Clement Mabina enzi za uhai wake. |
Mwenyekiti wa zamani wa Cha cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Bwana CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kali pamoja na kukata tamaa katiika eneo la Kisesa lililopo jijini Mwanza baada ya ugomvi kuzuka baina yao unaohusiana na kiwanja ambacho kesi yake ilikuwa ingali bado mahakamani.
Clement Mabina Akiwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye sherehe za kutimiza miaka 35 ya CCM |
Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa
kuwa yeye si msemajiwa jeshi hilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Habari zaidi zinasema kuwa
wananchi hao licha ya kesi kuwa kortini walimkuta marehemu akiliendeleza eneo
hilo na walipomhoji, akawatukana ikiwa ni pamoja na kurusha risasi hewani ndipo
walipopandwa na hasira kali wakaanza kumshambulia kwa mawe na vitu vyenye ncha
kali hadi wakamuua huku wapambe wake wakiingia mitini kuogopa na wao kukumbwa
na mauti.
Mwili wa Marehemu. |
Taarifa hiyo ya polisi ilieleza kwamba, mgogoro huo ulizuka baada ya wananchi hao kumtuhumu Mabina kuwa ana mpango wa kuuza eneo lao la kijiji kwa mwekezaji. “Ni mapema mno kuelezea tukio hili kwa undani hasa ikizingatiwa kuwa mimi siyo msemaji. Subiri msemaji wajeshi atawapa
taarifa kwa undani,” alisema ofisa huyo. Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime alithibitisha kutokea
kwa tulio hilo.
Chanzo Jamii forum
Chanzo Jamii forum
0 Response to "RAIA WALIOKATA TAMAA WAMUUA KWA MAWE KIGOGO WA CCM: NI CLEMENT MABINA WA MWANZA"
Post a Comment