Ikiwa Nchi ya Uchina leo hii itafanikiwa chombo chake cha anga za juu Chang’e -3 kutua salama katika umbo la angani lililokuwa karibu zaidi na Dunia yetu tunayoishi yaani Mwezi, nchi hiyo ya Mashariki mwa Dunia itakuwa Taifa la Tatu kurusha chombo na kikatua salama katika uso wa mwezi baada ya nchi za Marekani na Urusi kufanya hivyo miaka takribani 37 iliyopita.
Marekani ilikwenda mbali zaidi
kwani ilifanikiwa kurusha chombo cha Appolo 11 pamoja na binadamu waliokuwa hai ndani
yake wakafika huko na kurudi tena Duniani wakiwa salama wasalimini.
Change’s-3, chombo
kisichokuwa na binadamu ndani kikiwa kimebeba kigari(Rover) kinatarajiwa kutua
juu ya mwezi katika eneo liitwalo “Sinus Iridium” au “Bay of Rainbow” saa
kumi jioni kwa saa za huko China Desemba, 2014 kwa mujibu wa Shirika la Habari la China Xinhwa News.
Mara tu kitakapotua, Change’s-3
kitafyatua kigari chenye miguu minne kilichopewa jina la “YUTU” likiwa na maana
ya ‘Sungura’ kwa lugha ya Kichina, Kina kamera nne na miguu mingine miwili
iliyokuwa na uwezo wa kuchimbua chini ardhini umbali wa mita 30. Kitatalii juu
ya uso wa mwezi huku kikichunguza tabaka lake, udongo na miamba kwa angalao muda wa miezi 3.
Jina ‘Yutu’ lilichaguliwa
kwa kura na wananchi mtandaoni na linamaana itokanayo na hadithi ya kufikirika
ihusuyo mnyama Sungura mweupe wa “Mungu” aliyeitwa Change’s, na anayesadikiwa na
Wachina kwamba aliishi mwezini.
Uchina katika Misheni yake
hii iliyopewa jina la “China Lunar
Exploration Program” imegawanyika katika awamu tatu na ya kwanza ilikuwa ni
Kuuzunguka Mwezi, ya pili, Chombo kutua katika Mwezi na ambayo ndiyo hii ya
leo, halafu ya tatu itakuwa ni kuchukua
na kurudisha Duniani sampuli za udongo na mawe yanayopatikana mwezini ifikapo
hapo mwaka 2020.
Hii ni awamu ya pili na
awamu ya kwanza ilikuwa Change-1 na Change-2. China ina dhamira ya
kuudhibitishia ulimwengu uwezo wake kama Taifa kubwa sawa na Mataifa mengine ya
Magharibi kama Marekani.
Mataifa mengine ya mashariki yanayofanya jitihada katika safari na kutuma vyombo katika anga za juu ni India, Iran na Pakistan.
0 Response to "SAFARI YA KWENDA KUTUA MWEZINI: CHINA YAWA NCHI YA TATU BAADA YA MAREKANI NA URUSI"
Post a Comment