Mratibu wa Tamasha la Ujasiriamali, Abdallah Mrisho (wa pili
kulia) akiongea jambo na waandishi wa habari leo ndani ya ukumbi wa The Atriums
Hotel iliyoko Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
|
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (wa pili kushoto)
akiongea na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni mratibu wa tamasha hilo,
Abdallah Mrisho na kushoto ni H. Baba.
|
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). |
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Fid Q naye akielezea namna
atakavyolitumia tamasha hilo kuwajenga vijana wa Mwanza katika maisha yao
kupitia fani yake ya muziki.
|
Msanii kutoka jijini Mwanza, H. Baba, akielezea namna
alivyojipanga kuwafikishia somo la ujasiriamali wakazi wa Mwanza.
|
Baadhi ya waandishi na wapiga picha (kulia) wakichukua matukio ya
habari kuhusu tamasha hilo.
|
MENEJA
Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni mratibu mkuu wa Tamasha
la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii hadi Jumapili jijini
Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza kuhusu tamasha litakalofanyika siku ya
Ijumaa katika Viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mikakati yote
imekamilika.
Mrisho alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu
za mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa
kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali
za kujikwamua kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global
Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James Mwang’amba, Emmanuel Mgaya (Masanja
Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Kwa upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young
Killer, Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni
Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson
Mwasabwite.
(Habari/Picha: Musa Mateja / GPL)
0 Response to "SHIGONGO KUFICHUA SIRI ZA MAFANIKIO KWENYE UJASIRIAMALI IJUMAA-JUMAPILI CCM KIRUMBA MWANZA"
Post a Comment