SIKILIZA AUDIO YAKE HAPA CHINI.
Wimbo
huu Phenomene,
Mbilia Bel aliutoa mwaka 1997 baada ya
kuachana na marehemu Tabu Ley Rochereau na bendi yake ya Afrisa International
mwaka 1987. Ni wimbo wa kwanza alioufanya akiwa huru kiusanii na ulifanya
vizuri mno.
Mbilia
Bel tangu mwaka 1981 alijiunga na Tabu Ley katika bendi yake ya Afrisa
International ambapo kutokana na mvuto na uzuri wa ajabu aliokuwa nao mwanadada
huyo waliweza kuliteka vilivyo anga la muziki katika Bara zima la Afrika na nje
ya bara hilo kwa muziki wao wa Rhumba iliyochanganyika na Sokous hali
iliyosababisha hata bendi kongwe na maarufu kama TP OK JAZZ kuanza kupoteza mvuto na mashabiki waliokuwa nao awali.
Katikati
ya miaka hiyo ya 80, Mbilia bel na Tabu Ley Rochereau waliamua rasmi kuoana na
kuishi kama mume na mke huku wakiendelea kufanya kazi ya muziki pamoja mpaka
pale ndoa yao hiyo ilipokuja kuingiliwa na ‘kidudu mtu’ mwaka 1987.
Kama
ilivyokuwa kawaida kwa ndoa zote Duniani, matatizo yalitokana na wivu wa
kimapenzi baada ya Tabu ley kuamua kumleta kimwana mwingine mrembo (naye pia alikuwa mkali..!) kwenye bendi
aitwaye Kishila Ngoyi au kwa jina ka usanii Faya Tess kwa madai ya kwamba amsaidie Mbilia Bel katika safu ya
uimbaji. Hakuna kosa kubwa alilofanya Tabu Ley kama hilo, hakujua kama, ‘mwanamke
huweza huvumilia maudhi yote lakini siyo kumletea na kumuonyesha mwenzake hasa
ikiwa ni mzuri kama yeye au kumshinda’.
Mbilia
Bel akaanza kujawa na wasi wasi, labda Mzee Tabu anatoka out na Kishila
kinyemela, ndipo mapenzi na kazi vikaishia palepale. Aliachana na Afrisa
International pamoja na Tabu Ley akatimkia jijini Paris alipokwenda kujiunga na
mpiga gitaa maarufu Rigo Starr Bamundele ambapo albamu yao ya kwanza ilikuwa ni hii
Phenomene
na ilipata mafanikio makubwa.
Afrisa
International ya Tabu Ley baada ya kuhama kwa Mbilia Bel ilidorora na hata
idadi ya albamu zilizotoka ilipungua sana kutokana na Tabu Ley mwenyewe kukosa ile ari aliyokuwa nayo kabla, vile
vile kukosekana kwa mvuto wa Mbilia bel ambao mashabiki kote Barani Afrika na
nje walikuwa wameuzoea.
Picha hizi mbili hapa chini ni Mbilia bel alipokuja Tanzania na kufanya onyesho pale uwanja wa New World Cinema Mwenge jijini Dar. akiwa na Fally Ipupa.Picha na Michuzi blog.
Hebu angalia na kulinganisha picha tatu za mwanzo za Mbilia Bel na tatu zinazofuata za Kishila Ngoyi(Faya Tess) Je ni nani mkali kumshinda mwenzake?
Picha hizi mbili hapa chini ni Mbilia bel alipokuja Tanzania na kufanya onyesho pale uwanja wa New World Cinema Mwenge jijini Dar. akiwa na Fally Ipupa.Picha na Michuzi blog.
Kumbe Mbilia bel bado yumo pamoja na umri kwenda. |
Hebu angalia na kulinganisha picha tatu za mwanzo za Mbilia Bel na tatu zinazofuata za Kishila Ngoyi(Faya Tess) Je ni nani mkali kumshinda mwenzake?
MBILIA BELL.
KISHILA NGOYI (FAYA TESS)
0 Response to "SIKILIZA NA KUDOWNLOAD WIMBO MKALI PHENOMENE WA MBILIA BEL ALIOTOA AKIWA NA RIGO STARR BAADA YA KUACHANA NA TABU LEY 1987 "
Post a Comment