Majaji
BSS, Madam Rita Paulsen, Salama Jabir na Master J
|
“The X Factor ” ni mfululizo wa mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji
yanayofanyika nchini Uingereza na Marekani, mfano wa Bongo star Search, na
yaliyoasisiwa na Producer maarufu wa Televisheni aliye pia mjasiriamali mkongwe
Simon Phillip Cowell chini ya kampuni yake ya Syco
Nchini Uingereza yalianzishwa
mwaka 2004 wakati nchini Marekani yalikuja kuanzishwa mwaka 2011 Septemba 21,
mashindano haya hufanyika kuanzia miezi ya August/Septemba mpaka kufikia mwezi
Desemba na kama ilivyokuwa ‘Bongo Star Search’ hapa Bongo mashindano haya
hutawaliwa na mbwembwe za aina mbalimbali hasa za majaji wanaofanya kazi ya
kuangalia ni nani anayestahili kupita
miongoni mwa washiriki. Huonyeshwa katika luning za ITV ya Uingereza, na TV3 ya
Ireland kwa upande wa "The X Factor USA” Marekani mashindano haya
huonyeshwa katika Televisheni za Fox, CBS, SONNY na SYCOTV
Mmiliki
wa “The X Factor, Simon Cowell”
|
Mshindi kwenye “The X factor” hupatikana kwa kupigiwa kura na watazamaji wa Televisheni
kupitia simu na Intaneti na hatimaye mshindi huja kuzawadiwa fedha taslimu
pamoja na kupewa mikataba ya kurekodi katika Lebo ya Cowell mwenyewe.
Ukiwataza majaji wake
wakiongozwa na Simon Cowell mwenyewe ni kama vile walivyokuwa kina Madam
Rita, Master J.(Joachim Kimaro), Salama Jabir, na Kitime. Cowell ambaye ndiye
Jaji mkuu na mmiliki wa mashindano haya, amewahi pia kuwa jaji katika
mashindano mengineyo mengi yakiwamo, ‘Pop
Idol’, ‘Americans Got Talent’ nk.
Cowell
akiwa na Jaji mwenzake Cheryl Cole
|
Kama Jaji , Cowell
anafahamika sana kwa ukosoaji wake wa washiriki uliojaa lugha kali na hata
wakati mwingine kutukana, hali inayozua mjadala mkubwa. Pia anafahamika kwa
umahiri wake katika shughuli za Kimuziki na Televisheni. Amewahi kuibua vipaji
vya wasanii wngi wa muziki na watangazaji wa runinga, vilevile amewahi kutajwa
mmoja kati ya watu 100 wenye ushawishi zaidi Duniani mwaka 2004 na 2010.
Chanzo mitandao mbalimbali na wikipedia
Chanzo mitandao mbalimbali na wikipedia
0 Response to "WAONE "MAJAJI WA BSS" YA ULAYA/MAREKANI NI KAMA KINA MADAM RITA, SALAMA JABIR, KITIME NA MASTER J."
Post a Comment