Habari na Gazeti pendwa la TANURU LA FILAMU toleo la Dec.3
Mwanamuziki mkali wa Bongo
Flava Naseeb Abdul, ‘Diamond Ngololo Master’ wiki mbili zilizopita alikuwa
kikaangoni kwenye jamii baada ya kutupia kivazi kilichoonekana kumdhalilisha
zaidi ya kumpendeza, ilikuwa ni katika harusi ya mmoja wa ndugu wawili wa kundi
la P Square anayetambulika kama Peter Okoye.
Kwa kuvaa vazi hilo (suruali
ya zebra) Diamond aliambulia kashfa karibu wiki nzima ambapo kwa kujibu kashfa
hizo alifananisha kuvaa huko na mwanamuziki Whiz Khalifa ambapo pia wakali wa
mavazi waliweka wazi kuwa amechemka
kujifananisha huko.
Wengi walimshauri awe na mtaalamu wa mavazi badala ya
kujiamulia kuvaa tu. Baada ya kuwa gumzo karibu wiki nzima, gazeti hili
liliingia madukani kuulizia bei ya suruali hiyo mpaka isababishe kumdhalilisha
mkali huyo wa ‘mawazo’ “Hii suruali ndugu yangu tunauza kwa shilingi 55,000/-,
imepungua sana tutakuuzia kwa sh. 54,500/-, Alieleza John Ndeshau ambaye ni
mfanyabiashara maeneo ya Posta.
Gazeti hili halikuridhika, na kufanya ‘reseach’
katika maduka takribani matano na kugundua bei inacheza katika hizohizo
tulizoambiwa awali.,
Kwa mantiki hiyo Diamond
inawezekana akawa amenunua nguo hiyo kwa kiasi hicho cha fedha ambapo
ilimsababishia karaha wiki nzima.
Hapo kweli Umaikojakson ulimponza Diamond,
ReplyDelete