Tabu Ley na Mbilia Bel |
Miaka ya 80
Kenya ilipokuwa na stesheni moja tu ya redio ‘Sauti ya Kenya’ iliyokuwa
ikimilikiwa na Serikali, iliamua kuzipiga marufuku nyimbo zote za nje kuchezwa
katika redio hiyo.
Haraka, Tabu Ley Rochereau alitunga kibao kikali na kitamu cha muziki kilichojulikana kama ‘Twende
Nairobi’ na ambacho kiliimbwa na aliyekuwa mkewe Mrembo Mbilia Bel. Kibao hiki
kizuri kilimsifia rais Moi na mara moja kikaupoza moyo wa rais na akabatilisha
mara moja marufuku iliyokuwa imewekwa.
Kubadilisha msimamo wa Rais hasa nyakati zile za chama
kimoja haikuwa jambo rahisi, lakini kwa wanamuziki wa Kongo (Zaire) wa kipindi
kile walikuwa na uwezo huo, kwani hata Marehemu Luambo Luanzo Makiad naye
inasemekana kuna wakati aliuteka sana moyo wa aliyekuwa Dikteta wa nchi hiyo
Marehemu Mobuttu Seseseko.
Tabu Ley Rochereau enzi za uhai wake akiwa na mpenzi wake Mbilia bel |
Tabu ley jana
alifariki Dunia akiwa katika hospitali
moja nchini Ubelgiji alikokuwa amelazwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi
ya kisukari na kiharusi kilichompata mwaka 2008.
Atakumbukwa kwa nyimbo zake
kali zaidi ya 2000 ukiwemo uliompatia chati ya juu sana, MUZINA pamoja na album
zipatazo 250, huku akiwa ameibua vipaji kibao vya wanamuziki wengine akiwemno
aliyewahi kuwa mke wake Mwanadada mrembo Mbilia Bel
Hebu sikiliza audio ya wimbo hapa na
kuona video ya kibao hicho,Twende Nairobi, Nakei Nairobi;
Audio, wimbo wa Twende Nairobi uliomfanya Rais Moi wa Kenya anywee ghafla
Audio, wimbo wa Twende Nairobi uliomfanya Rais Moi wa Kenya anywee ghafla
VIDEO YA TWENDE NAIROBI.
0 Response to "TWENDE NAIROBI WA TABU LEY NA MBILIA BEL WIMBO ULIOBADILISHA HARAKA MSIMAMO WA RAIS MOI KENYA"
Post a Comment