Mnyama
Simba akinyeshewa mvua huku amejikunyata utafikiri ni paka vile
|
Mengi yalisemwa na
mashabiki wa pande zote mbili Yanga na Simba, kila mmoja akijitutumua kwamba ni
lazima mechi ya leo angeibuka na ushingi, lakini kauli ninayoikumbuka vizuri zaidi
ni hii ya shabiki mmoja wa Timu ya Simba
aliyekuwa akiwaambia wenzake, mashabiki wa timu ya yanga kwamba “Usimuone Simba
kalowa ukadhani ni paka atakurarua”
Jamaa huyo alikuwa
akijibu mashambulizi ya wapinzani wake waliokuwa wakijitapa kuwa Simba ya sasa
si lolote si chochote kwani imegubikwa na migogoro isiyoisha, wachezaji wana
njaa, na wachezaji kama kina Okwi na Juma Kaseja waliokuwa Simba zamani wakaja
kuhamia Yanga wangeweza kufanya maajabu kwa kuiadhibu Simba kama mtoto mdogo.
Matokeo yake imekuwa “vais vesa” kumbe hakuwa paka ni Simba yule yule wa siku
zote.
0 Response to "UKIMWONA SIMBA KALOWA MVUA USIDHANI NI PAKA"
Post a Comment