Serikali kupitia Ofisi
ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania
wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili
ya waajiri mbalimbali Nchini.
Daudi alitaja nafasi
za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja
la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii,
Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa
utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu
Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo
msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni
Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti
daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa
kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja
la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi
wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii,
mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii na Afisa vipimo.
Kwa mujibu wa Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara
ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya
Kinondoni.
Nafasi nyingine ni kwa
ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi,
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.
Nafasi hizo pia ni kwa
ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.
Waajiri wengine ni
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu. Kwa maelekezo zaidi tembelea hapa katika tovuti ya serikali ya ajira
0 Response to "UNGEPENDA NAFASI YA AJIRA/KAZI SERIKALINI?"
Post a Comment