Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini |
Wachambuzi wa mambo
wamedai ya kwamba inawezekana kabisa kutokana na Afrika ya Kusini hususan
katika chama cha ANC kuwepo mivutano iliyosababisha kuanzishwa kwa vyama
vingine pinzani kama kile kilichoanzishwa na Julius Malema aliyekuwa kiongozi
wa vijana ANC akatimuliwa kwa utovu wa nidhamu basi inawezekana waliofanya
kitendo hicho wakawa miongoni mwa hao wasioridhishwa na uamuzi wa chama kumtema
Julius Malema.
Ilibidi Askofu
mstaafu wa Anglican na mshindi mwenza na Mandela wa tuzo ya Nobel ya Amani Askofu
Desmond tutu wakati akitoa hotuba yake atumie busara ya hali ya juu, kwa
kutanguliza kwanza rai kuwa yeye anasimama kama mzee na angeomba watu wote
wliofika pale kuwa na heshima na staha kwa wageni waliokuwa wamefika pale.
Kweli bwana kumbe utu uzima ni dawa watu mara moja walitii kauli ya Mzee Tutu
wakanyamaza na alipowaamuru kusimama walifanya hivyo kwa adabu.
Ingawa kuna raia
wengi wa Afrika ya Kusini wasioridhishwa na mienendo ya Taifa hilo hasa baada
ya Mandela kuachana na ulingo wa siasa lakini hapana shaka kwamba asilimia
kubwa ya Waafrika Kusini bado wana imani kubwa na chama chao cha ANC, pamoja na
Jacob Zuma mwenyewe.
Wazomeaji wanaweza
kuonekana washindi katika hafla hiyo tu
lakini katika mustakabali wa siasa za Afrika ya Kusini chini ya misingi imara aliyoiasisi,
mwenyewe Marehemu Nelson Mandela hawana
chao. Iweje kweli kama una akili timamu na unataka kumuenzi mtu unayemheshimu
kwa kujali uvumilivu, haki,amani na upendo, ukaanze kuzomea kwenye umati wa
watu mashuhuri tena katika shughuli ya maombolezo ya mtu aliyechukia uhuni wa
dizaini hiyo.
Hivi kweli ule ni ustaarabu? Hata hapa kwetu Tanzania tabia kama
hiyo ipo kwa baadhi ya watu kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.
0 Response to "WAFUASI WA MALEMA WAMZOMEA RAIS JACOB ZUMA WAKATI AKIHUTUBIA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO YA MZEE MANDELA"
Post a Comment