![]() |
Aina mbalimbali za soda. |
Lakini
ni kitu gani kinachosababisha kinywaji hiki kuwa na sifa hizo? Kwenye soda hasa
zile za Cola huwekwa kemikali, Asidi aina ya Citric, ambayo ndiyo chanzo cha
kuwa na uwezo huo wa kumengenya vitu kiasi hicho. Lakini ikumbukwe kuwa acid
hiyo haipatikani katika soda tu peke yake, kwani kumekuwa na watu wapotoshaji
wanaotangaza ubaya wa soda kama kwamba ni kitu hatari zaidi kushinda vitu au
vyakula vingine vilivyokuwa na kemikali hii ya citric acid.
Vyakula
vingine ambavyo siyo soda lakini ndani yake vina asidi hii ni pamoja na matunda
kama vile machungwa malimao, ubuyu, ndimu, ukwaju na hata soda zisizokuwa za
cola. Kinachotofautisha soda za cola na zile zisizokuwa za cola ni kiwango tu
cha citric acid iliyoko ndani yake, vya cola vina acidi nyingi zaidi.
Tunapozungumzia
madhara yatokanayo na asidi ya soda za cola ni lazima tujiulize kwanza ikiwa
citric acid yenyewe ni hatari kwa kiasi gani katika miili yetu, na ikiwa basi
ni hatari je, vyakula vingine vyenye hii acid siyo hatari? Kwa hiyo na
machungwa nayo tuyapige vita? Au citric ya matunda na ile ya kiwandani
inayotiwa katika soda huwa zinatofauti fulani?
Kwa
mujibu wa wataalamu wa kemia wanasema kwamba kemikali ya citric acid,
imeunganishwa na atomi nyingi za Hydrojeni na hivyo kuifanya iwe rahisi mno
kuyeyuka katika maji jambo linaloifanya isihifadhiwe mwilini kwa muda mrefu.
Wanasema ili citric acid iweze kuwa sumu basi inabidi kiwango kikubwa sana cha
kemikali hii kiingizwe mwilini kwa mara moja ndipo kiweze kuleta madhara.
![]() |
CHUNGWA NA NDIMU. |
Kimsingi
wanasema kwamba citric acid ndiyo vitamin C yenyewe na inahitajika sana kwenye
miili yetu katika kusaidia mfumo wa kinga za mwili “immune system” lakini
inahitajika tu katika kiwango cha kadiri, nyingi zaidi inaweza ikaleta madhara.
Tukiachana
na madhara yanayoweza yakasababishwa na citric acid kwa ujumla inapotumiwa
katika kiwango kikubwa, yapo madhara mengine ambayo watu hawaelewi ni makubwa
hata kushinda vile wanavyodhania kwamba husababisha ndani ya miili yetu.
Kuyeyusha
meno! Acidi hii ina uwezo mkubwa wa kuyeyusha vitu vyenye asili ya chokaa kama
meno na hata vitu vya asili ya chuma ndiyo maana watu wengi wamekuwa
wakionyesha madhara yake kwa kusema “unapoweka msumari ndani ya chupa yenye
cola siku kadhaa basi ukija kuuangalia huukuti tena”
Sina
uhakika na hilo lakini ni kweli kwamba citric acid inao uwezo wa ‘kula’ vitu
vya chuma. Kuyeyusha msumari mzima mzima sijafanya utafiti kujua inachukua muda
gani. Kuna wataalamu wengine wanaodai kwamba uwezo wa citric acid kusaga vitu ni karibu sawa na ule
wa acid za maji ya betri na uwezo wa acid iliyoko ndani ya vinywaji vya cola ni
mara 10 zaidi ya ule uliokuwa katika soda za kawaida. Lakini cha kustaajabisha
zaidi ni kwamba ingawa soda za kawaida zina asidI kidogo kushinda zile za cola
lakini zinasaga meno vizuri zaidi kushinda zile za cola.
Wakati
acid za kwenye betri zina PH (kipimo cha asidi na alkali) namba 1.0, maji ya
kawaida ambayo ni “neutral”,si acid wala alkali yana PH ya 7.0, soda za cola
zina PH ya 2.5 wakati soda za kawaida ni 4.0. Katika utafiti uliofanyika mwaka
2006 ulibainisha pia kwamba acid kwenye machungwa nayo husababisha meno
kumongonyoka lakini si kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwenye soda. Kwa
ujumla vinywaji vyote vinavyosindikwa viwandani huwekwa acid ambazo ni hatari
kwa meno na ikiwa unajali meno yako na ungependa yabakie kuwa salama kwa muda
mrefu basi ni kuvikwepa ama kutumia kwa kiwango kidogo sana.
![]() |
JUISI HALISI YA MATUNDA |
Richard
Adamson Mwanasayansi mshauri kwenye taasisi inayojihusisha na vinywaji ya
Marekani akiongea na jarida la “Live
science” alisema hivi; “kinga kubwa uliyokuwa nayo mdomoni kwako ni mate
ambayo hupoza acid, vipo vyakula vingi na siyo soda peke yake vinavyoweza
kuozesha meno kama baadhi ya matunda, hakuna kigezo kimoja. Kinachotakiwa hapa
tu ni kufurahia kila kitu kwa kadiri”.
Anatoa ushauri kwa watu kutumia mirija “Straws”
wakati wanapokunywa soda ili kupunguza ile hatari ya soda kugusana na meno na
anasema njia ya kupunguza matumizi ya soda ni kwa kunywa soda wakati wa
chakula.
CHANZO:
Mitandao mbalimbali.
0 Response to "HATARI! SODA ZA COLA HUYEYUSHA MISUMARI, MENO NA BETRI ZA MAGARI"
Post a Comment