Ile dhana kwamba watu
waliofanikiwa katika maisha, iwe ni katika uchumi, usanii au katika Nyanja nyingineyo
yeyote ile ya maisha, kwamba hawapendi kutoboa siri za wao kufikia pale walipo
au hata kuwasaidia watu wengine hata kimawazo ili na wao waweze kuondokana na
hali duni, inazidi kupingwa na watu mbalimbali mashuhuri kuwa siyo kweli baada
ya msanii maarufu wa kike Afrika mashariki Lady J D kuibuka na kusema katika
ukurasa wake wa Face book kuwa yeye siyo mchoyo wa kushirikiana na wasanii
wengine wanaoinukia.
Jaydee aliwauliza mashabiki
kwamba, ni nani anasema yeye ni mchoyo wa ‘kolabo’? huku akiorodhesha nyimbo
zipatazo 30 anazodai kufanya na wasanii mbalimbali wan nje na ndani ya
Tanzania, “Nina uhakika kabisa kuwa kuna
nyingine nimezisahau” aliongeza Binti machozi aka ‘Komando’.
Hapo awali wasanii wadogo
walikuwa wakimtuhumu Lady J. D kuwa huwanyanyapaa katika kufanya nao kolabo na
mmoja wa wasanii hao waliowahi kutoa malalamiko yao ni yule aliyeimba wimbo wa ‘Bonge
la bwana’
0 Response to "JAYDEE: SIFICHI SIRI ZA MAFANIKIO YANGU WALA SINA UCHOYO KWA UNDERGROUNDS"
Post a Comment