![]() |
Wasichana wakipokea simu ofisini. |
Kupokea
na kupiga simu katika biashara hata kama ikiwa ni biashara ndogo vipi siku hizi
imekuwa ni jambo la lazima kama mjasiriamali atataka mafanikio ya kweli tofauti
na zamani ambapo kwanza simu zenyewe zilikuwa ni akama bidhaa ya anasa na
wakati mwingine kwa wale waliokuwa na vipato vikubwa tu.
Kwa
mantiki hiyo simu na hasa za mkononi zimekuwa ndiyo mawasiliano ya msingi
kabisa baina ya mwenye biashara na wateja wake hivyo kusababisha kuwepo na
umuhimu mkubwa wa wajasiriamali kufahamu njia na mbinu bora za kupokea simu
pindi wateja wanapopiga kuhitaji msaada ama bidhaa fulani.
![]() |
Rais Obama akipokea simu. |
1) Usicheleweshe
kupokea simu pindi inapoanza kuita,jitahidi angalao isiite zaidi ya mara mbili.
2) Unapopokea
simu, mkaribishe anayepiga kwa upole na shauku ya kutaka kujua shida yake, usisahau
kuwa hapa sauti yako ndiyo kila kitu katika kuchora picha nzuri ya
biashara/kampuni yako. Mathalani unaweza ukasema, “Habari za saa hizi, Mariam
Beauty Saloon, Mariam naongea. Nikusaidie nini tafadhali?” Unamtambulisha
kwa sababu asingekuwa na haja ya kupiga simu ikiwa tayari alikuwa na taarifa za
biashara yako.
3) Zungumza
taratibu na kwa ufasaha lakini isije ikawa taratibu kupita kiasi mteja wako
akashindwa kuelewa kile unachomwambia kwa urahisi.
4) Usitumie
maneno ya mtaani, au maneno yasiyoeleweka kwa urahisi, wala usitumie misamiati
ya kitaalamu ikiwa huna uhakika kwamba yule unayezungumza naye yupo katika
sekta husika.
5) Tumia
lugha chanya kwa mfano badala ya kusema “sijui” sema “Nitajaribu kutafuta jibu”
6) Hakikisha
unapokea ujumbe uliokamilifu na sahihi, kama kuna neno hujalielewa sawasawa au
labda ni jina la mtu, muombe akutajie tena au akutajie herufi zake.
7) Usiahirishe
kujibu simu mpaka kesho au siku nyingine, kwani waweza kupoteza tenda muhimu au
mauzo ambayo ungeyafanya endapo ungewahi.
8) Ukiona
kuna tatizo katika kupokea simu usisije ukamweka hewani pasipo majibu “on hold”,
mjulishe kwa ripoti kwamba simu iko bize, kama ataendelea kusubiri au asubiri
mpaka baadaye umpigie tena.
9)
Usiweke “loudspeaker” labda tu kama ni lazima
kufanya hivyo. Mteja anaweza akawa na fikra kwamba hauko makini na simu yake,
haumjali na unataka kila mtu ajue ni nini anachozungumza hivyo ujumbe wake siyo
siri tena.
10) Mfundishe
mtu mwingine yeyote anayehusika katika biashara yako
namna
bora ya kujibu simu, anaweza akawa ni msaidizi wako, mfanyakazi, au wanafamilia
ikiwa biashara inafanyikia nyumbani. Fanya majaribio kwa kujifanya mteja kisha
ukawapigie kujfahamu kama wameelewa vizuri namna ya kujibu simu au la.
0 Response to "JIBU SIMU KIBIASHARA:JIFUNZE MBINU BORA ZA KUPIGA NA KUPOKEA SIMU"
Post a Comment