Kisiwa kikiota kama uyoga
|
Kisiwa
hicho kinachoota mithili ya uyoga na kuongezeka ukubwa kila dakika inayopita,
kimewaacha watu wengi midomo wazi kutokana na kila dakika kubadilika umbo. Kisiwa
hicho kimeibuka kilomita 1,000 Kusini mwa jiji kuu la Tokyo miezi 2 iliyopita
baada ya mlipuko wenye nguvu wa volcano kutokea chini ya bahari hiyo ya Pasific.
Wachambuzi wa mambo tayari wameshasema kwamba kisiwa hicho kinaweza kikaongeza
zaidi ukubwa wa nchi hiyo ya Japan katika eneo la bahari maalumu kiuchumi.
Kisiwa kipya kikiungana na cha zamani. |
Kwa
mujibu wa shirika la “NASA” la Marekani, uhunguzi waliofanya angani katika eneo
hilo umebainisha kuwa Volcano ya chini ya bahari kwa mara ya mwisho katika eneo
hilo ililipuka tena mwaka 1973 na 1974. Kisiwa kinachoishi watu kipo kilomita
130 au maili 80 kutoka kilipo hiki. Wakati Wajapan wengi wanaishii katika
visiwa vinne vikubwa zaidi, Taifa hilo linaundwa na takribani maelfu ya visiwa
vidogovidogo vilivyotapakaa huku vingine vikiwa katika mgogoro na Taifa jirani
la Uchina.
0 Response to "MAAJABU: KISIWA KIPYA CHAOTA BAHARINI KAMA UYOGA"
Post a Comment