Lesego Motsepe enzi za uhai wake |
Aliyekuwa
muigizaji mashuhuri wa Tamthiliya ya “Isidingo
The Need” “Lesego Motsepe” miaka 39 amefariki dunia baada ya kupambana na
Virusi vya Ukimwi kwa takribani muda wa miaka 15.
Akijulikana
kwa jina la Ustaa la ‘Letti Matabane’ tangu mwaka 1998 hadi mwaka 2008 ‘Lesego’
alifanya kazi ya uigizaji, sambamba na kutoa ‘speech’ za kuwatia watu moyo na
kuhamasisha, “motivational speeches” vilevile alikuwa ni balozi wa Ukimwi.
Alijitangaza
rasmi kuishi na virusi vya ukimwi siku
ya ukimwi Duniani hapo Desemba 1 2011 na
kusema kuwa alikuwa akiishi na hali hiyo
tokea mwaka 1998.
Aliacha
matumizi ya dawa za kurefusha maisha ‘ARVS’ kinyume na ushauri wa daktari wake
hapo July 2012 kwa madai kwamba alikuwa anataka kuhamia kutumia dozi takatifu
“Holistic regimen” yaani tiba kwa njia ya tafakuri au “Meditation”, matumizi ya
mitishamba, “Beetroot diet” pamoja na kula vitunguu swaumu.
Alisema
kwamba asingeweza kuendelea na wazo la kutumia ‘ARVS’ katika muda wa maisha
yake wote uliokuwa umesalia.
0 Response to "MUIGIZAJI ALIYEACHA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA ARVS AFARIKI DUNIA"
Post a Comment