MWANASOKA EUSEBIO DA SILVA FERREIRA NI KAMA EDSON PELE, MUHAMMAD ALI NA MICHAEL JACKSON | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MWANASOKA EUSEBIO DA SILVA FERREIRA NI KAMA EDSON PELE, MUHAMMAD ALI NA MICHAEL JACKSON

Eusebio Da Silva Ferreira, 
akisakata kabumbu enzi za uhai wake 
Katika Nyanja ya michezo duniani, na hususani mpira wa miguu, ndondi na muziki, hauwezi ukaizungumzia pasipo kuwataja watu hawa watatu mashuhuri weusi waliokuwa na asili yao katika Bara la Afrika.

Hii inathibitisha ile dhana  kwamba watu wenye vipaji vya hali ya juu wengi katika michezo na hata burudani asili yao ni kutoka katika bara la Afrika. Tukiwa tunaomboleza kifo cha mcheza soka mashuhuri aliyewahi kutokea duniani Eusebio da Silva Ferreira, raia wa nchi ya Ureno lakini aliyezaliwa katika Taifa masikini kabisa la Msumbiji, tunatakiwa pia tutafakari na michango ya watu wengine weusi duniani waliowahi kufanya mambo yakushangaza na ambayo ni watu wachache mno ama hata mengine hakuna na pengine haitatokea tena binadamu mwingine atakayeweza kuzivunja rekodi walizoweka.

'Eusebio' mwanasoka mashuhu.ri wa wakati wote
Kama ilivyokuwa kwa Bondia Muhammad Ali, katika tasnia ya mchezo wa ndondi, anatajwa kwamba ndiye bondia maarufu na mahiri zaidi Duniani kuwahi kutokea. Hii ina maana kwamba, umaarufu wake ni wa vizazi vyote.

“Edson Arantes Pele” wan chi ya Brazil naye katika mchezo wa soka anatajwa kuwa ndiye mfalme wa soka, Duniani, na sifa na ushujaa wake aliouonyesha katika mchezo huo havitakaa vifikiwe na mtu mwingine yeyote. Hali kadhalika katika muziki Mfalme wa Pop Duniani Michael Jackson aliye pia na asili yake barani Afrika sifa na umahiri wake katika tasnia yake hiyo, ni vigumu akatokea mtu Duniani milele na milele akaja kumpiku. Kutokana na umahiri wake huo walimpa jina la "Black Panther" lenye maana ya 'Chui mweusi' 
'Edson Pele' wa Brazil, mchawi wa soka Duniani.
‘Eusebio da Silva Ferreira’ aliyefariki dunia Jumapili ya tarehe 5 January 2014 kwa maradhi ya moyo akiwa na miaka 71, alizaliwa nchini Msumbiji wakati wa vita ya pili ya Dunia ambapo baada ya kuonyesha uhodari mkubwa katika timu aliyokuwa akichezea huko Msumbiji hatimaye timu ya ‘Benfica’ ya Ureno(wakati huo ureno ikiitawala Msumbiji) iliamua kumchukua akiwa na umri wa miaka 18 pekee.
 
"Michael Jackson" mfalme wa Pop Duniani
Miaka ya 60, alifanya maajabu makubwa pale alipoiwezesha timu yake ya Benfica kuifunga ‘Real Madrid’ mabao 5-3 ushindi ulioiwezesha kushika nafasi ya pili katika ligi ya bara hilo. Mwaka 1966, alifanya maajabu mengine pale alipoiwezesha timu yake ya Taifa kuichabanga timu ya Taifa ya Korea ya Kaskazini mabao matano muda mfupi tu baada ya Korea kuwa ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3, hii ilikuwa ni katika kombe la Dunia. Mwaka 1965 vilabu vya Italia vilitaka kumnunua kwa gharama yeyote ile lakini kiongozi wa Ureno wakati huo Dikteta “Antonio Salazars” akatangaza kuwa Eusebio alikuwa  ni hazina ya Taifa na hivyo isingewezekana kabisa auzwe nje ya nchi.


"Eusebio Da Silva"
Mwaka 1998, Jopo la wataalamu 100 lililokusanywa na 'FIFA' lilimtaja Eusebio mmoja kati ya watu 10, mashuhuri zaidi Duniani kwenye mchezo wa soka katika maisha yote. “Angalia, tupo watu wawili tu weusi kwenye listi: mimi na Pele” Eusebio alikuwa akisema hayo, akimaanisha mwanasoka mwingine mashuhuri kutoka nchi ya Brazili, Edson Pele na ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa. “Nachukulia hilo kama jukumu kubwa kwa kuwa naiwakilisha Afrika na Ureno ni nchi yangu ya pili” alisema Pele. 

0 Response to "MWANASOKA EUSEBIO DA SILVA FERREIRA NI KAMA EDSON PELE, MUHAMMAD ALI NA MICHAEL JACKSON"

Post a Comment