Rais Barack Obama na mkewe Michelle
|
Rais Vladmir Putin na mkewe kabla hawajatengana.
|
Jarida la National Enquirer
lilieleza kwamba katika moja ya matukio, Obama aliwahi kukutwa akiwa na
mwanamke mwingine katika ‘mazingira ya kutatanisha’ wakati mkewe akiwa
safarini.
Kutokana na ripoti iliyotolewa
na Bombshel , Michelle na Obama wamekuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya
Ikulu. Michelle pia anajiandaa kuhama katika jumba lao pale Chicago ambalo
wameishi wakati wa uchumba wao miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo watajadili
juu ya talaka.
Taarifa ilidai tatizo limeanza
miaka minane iliyopita pale Obama alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao
Sasha ambaye aliumwa ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal
Meningitis ndiyo uliowafanya waendelee kuwa pamoja.
Kitabu cha Anderson kinaelezea
tatizo lilivyoanza baada ya Barack Obama kuamua kuingia kwenye siasa, ambapo
Michelle alisikika akimwambia mumewe; “Wewe unajifikiria mwenyewe tu.”
Naye Barack Obama amesikika
akisema: “Sikuwahi kufikiri kamwe kwamba ningelea familia mwenyewe siku moja.”
Anderson anadai kuwa Obama amechoshwa na malalamishi ya mkewe.
“Nampenda sana Michelle lakini
ananiumiza na ubishi wake wa kila mara,” alisikika akisema Obama na kuongeza
kuwa; “Anaonekana ni mwingi wa machungu na hasira siku zote.”
Akizungumza na televisheni ya
CBS ya Marekani, Anderson alidai kuwa ilikuwa nusura Michelle atembee nje ya
ndoa kwa sababu ya upweke.
Kwa miaka mitano wamekuwa na
wasiwasi juu ya uwezo wao wa kupata watoto kabla Malia hajazaliwa.
Walishajadili sana suala la kuasilia watoto (adoption) na marafiki zake wa
karibu lakini kwa bahati nzuri Malia alizaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.
Jina kamili la Obama ni Barack
“Barry” Hussein Obama, Jr, alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia
huko huko Hawaii na Indonesia, baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili
la mkewe ni Michelle LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964 Chicago,
Illinois.
Kukutana kwako
Barack na Michelle walikutana
mwaka 1989 katika mazingira ya kikazi, walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika
Kanisa la Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois.
Lakini vyanzo vingine vya
taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara, hasa baada ya tukio la Obama kupiga
picha za pamoja bila aibu na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt
(46) wakati wa mazishi ya aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrka Kusini, Neslon
Madiba Mandela.
Obamaakimpiga
piga begani waziri mkuu wa Denmark
|
“Lakini kwa sasa Michelle
anajiona kanyanyasika na kuaibishwa mbele ya dunia kwani picha hizo zilirushwa
duniani kote kupitia televisheni, magazeti na mitandao mbalimbali. Alisikika
akimtapikia Obama huku akisema “Nimechoshwa.”
Pia tatizo limekuzwa na safari
ya kikazi ya Obama hivi karibuni kule Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri
Mkuu mrembo kuliko pengine wote duniani , Yingluck Shinawatra.
Tarifa zaidi zilieleza kwamba
usalama wa taifa nchini humo unafahamu kuhusu suala hilo, lakini umekuwa
ukilichukulia kama suala binafsi na Michelle alionekana kukasirishwa kupita
kiasi alipopata taarifa hizo.
“Baada ya tukio hilo Michelle
aliamua kuwasiliana na mwanasheria wake akitaka kujua namna ya kuomba talaka na
alimwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye,” ilieleza sehemu ya
taarifa hiyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa
makubaliano waliyofikia, ilielezwa kwamba Michelle ataendelea kuishi mjini
Washington DC hadi binti yao mdogo, Sasha (12) atakapomaliza elimu yake ya
sekondari. Binti yao mkubwa, Malia (15) tayari ameshaingia sekondari.
“Michelle (50) kwa sasa
ataendelea kuishi kwenye Ikulu ya Washington hadi Obama atakapomaliza muda wake
wa urais ili tu aweze kuonekana kama yupo, lakini aliweka wazi kabisa kwamba
wataishi maisha tofauti,” ilieleza ripoti hiyo ikimkariri mmoja wa vyanzo
kutoka Ikulu hiyo. Ripoti hiyo ilikariri chanzo hicho kikieleza; “Michelle kwa
sasa anaishi katika vyumba vya watumishi kwenye nyumba yao ya familia na
anajiandaa kuchukua vifaa vyake na kuvipeleka kwenye nyumba yao binafsi ya
Chicago”.
Taarifa nyingine ilieleza
kwamba tayari mambo baina ya wanandoa hao yameshakuwa magumu kiasi kwamba
wamekuwa wakiishi kwenye vyumba tofauti katika Ikulu ya Marekani.
Mgogoro wao
Barack na Michelle wamekuwa
katika mgogoro kwa miaka kadhaa na wanalazimika kuwepo pamoja kwa sababu tu ya
watoto wao na kulinda hadhi yake kisiasa. Lakini kwa sasa Michelle amekuwa
mkali kweli kweli. Anaona kama amepuuzwa na kudhalilishwa mbele ya dunia nzima
na amekuwa akipiga kelele akisema, “Nimevumilia vya kutosha”, taarifa zaidi
zilieleza.
Obama na Michelle wakionekana haapikiki tena chungu kimoja
|
“Kwa sasa Barack anaonekana
kama amemwaibisha Michelle mbele ya dunia na kwa hili ni wazi kwamba atalilipa
kwa gharama kubwa,” kilieleza chanzo kutoka Ikulu ya Marekani.
“Ni jambio lililo wazi kwa sasa
kwamba Michelle ameshamwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye,
japokuwa kwa sasa imekuwa ni suala gumu kwa kuwa anahitaji aendelee kuonekana
wakiwa pamoja kwa sababu muhimu, lakini wanapokuwa nyumbani wanaishi maisha
tofauti ya kutengana,” kilieleza chanzo hicho.
Iwapo taarifa hizo ni sahihi,
hii inamaanisha kwamba Michelle ameudhika kupindukia na hii si mara ya kwanza
jambo hilo kutokea miongoni mwao.
Tangu Obama alipochaguliwa kuwa
rais, vitabu viwili vimemtaja vikidai kwamba wenza hao walikaribia kutengana
katika kipindi cha miaka yao ya mwanzo ya ndoa na hata Michelle alifikia hatua
ya kutaka kuomba talaka akidai kwamba anaona maisha yake ya kisiasa yanawanyima
furaha na kuwa pamoja nyumbani.
Mwaka 2009 mwandishi wa siku
nyingi wa Washington, Richard Wolffe alisema kwamba ndoa hiyo ilikuwa sawa na
iliyovunjika miaka tisa kabla kutokana na harakati za kisiasa za Obama
zilizokuwa zikimsababisha asiwe karibu na familia kwa muda mrefu.
“Kulikuwa na mawasiliano kidogo
sana na familia yake na hata mapenzi yalipungua. Michelle alikasirishwa sana na
hali hiyo akilaumu kwamba mumewe anaonekana kuwa mbinafsi; ilimpa wakati mgumu
sana,” aliandika Wollfe.
Wakati huo Michelle alilazimika
kutulia kwa kuwa tayari alishakuwa mama, mbinti zao awili, Malia na Sasha kwa
sasa wana miaka 15 na 12. Mumewe ambaye walikutana kwa mara ya kwanza
walipokuwa wakifanya kazi kwenye shirika moja la sheria mjini Chicago mwaka
1989, alikuwa ndiyo kwanza amechaguliwa kuwa Seneta wa Illinois na alikuwa
akijipanga pia kuwania nafasi kwenye baraza la Congress.
Mke wa Rais wa zamani wa
Ufaransa, Nicolas Sarkozy, Carla Bruni alipoulizwa katika moja ya vitabu kuhusu
uzoefu wake wa maisha ndani ya Ikulu alijibu, ‘Acha kabisa! Usiulize ni kama
jehanamu. Sikuwahi kuyafurahia’ ambapo Michelle alisema hakuwahi kuzungumza
maneno ya aina hiyo.
Mwaka 2012 mmoja wa waandishi
wa masuala ya siasa, Edward Klein alieleza kwamba Obama alionekana mwenye
mawazo kupita kiasi, wakati ndoa yake ilipokuwa kwenye matatizo mwaka 2000
kiasi kwamba rafiki zake walihofu kwamba anaweza kujiua.
Alieleza kwamba Michelle
alikuwa mwenye hasira kwa kuwa alimkataza Obama kuwania nafasi kwenye Congress,
ushauri ambao hakuufuata na hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi.
“Baada ya kushindwa alirejea
kwa Michelle kwa ajili ya kupata pumziko. Lakini Michelle hakuwa tayari
kuonyesha huruma yoyote,” aliandika Klein aliyedai kwamba marafiki wa Michelle
walimweleza kuwa tayari ameshafungua kesi akidai talaka.
Chanzo cha habari ni MWANANCHI.
Hivi karibuni Rais wa Taifa Kubwa na
lililokuwa na nguvu sawa na Marekani kipindi cha vita baridi miaka ya 90 na
kabla ya hapo Urusi, Rais Vladmir Putin naye waliachana na mke wake kwa kupeana talaka
kwa amani kabisa huku wakifanya sherehe. Putin na mkewe Lyudmila Skrebneva ndoa
yao medumu ka miaka 30 na imeelezwa kwamba kama ilivyokuwa kwa akina Obama na Michelle, chanzo cha ndoa yao kuvunjika ni mwanamke kutoridhika na majukumu mengi
aliyokuwa nayo mumewe. Aliwahi kusikika akisema kwamba “Putin ni kama kaolewa
na kazi yake” Vile vile nao wana watoto wawili wa kike ‘Maria’ na ‘Yekaterina’
0 Response to "NDOA YA OBAMA NA MKEWE TIAMAJI TIAMAJI KUSAMBARATIKA KAMA YA PUTIN WA URUSI"
Post a Comment