Tume hiyo imesema kuwa
matamshi ya Bwana Raila ni hatari na kwamba yanaweza kuzua vurugu na hivyo
kumtaka kuomba radhi mara moja.
Aidha tume hiyo
imemtaka Raila kutoa ushahidi wa madai yake la sivyo atake msahama tume hiyo.
''Licha ya kuwa uchaguzi ni siasa, matamshi ya Raila ni siasa mbaya,'' ilisema
taarifa ya tume hiyo.
![]() |
Rais Uhuru na makamu Rutto
|
Raila alitoa matamshi
yake katika muhadhara wa wafuasi wake katika jimbo la Kisumu Magharibi mwa
Kenya ambako anatoka.
Tume ya uchaguzi
inahoji kwa nini Raila hakutoa malalamiko hayo kama ushahidi wake wakati wa
kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mwaka jana badala ya kutoa matamshi mwaka
mmoja baadaye.
Odinga aliwania uchaguzi
kama Rais mwaka 2013 mwezi Machi ingawa alishindwa na punde baadaye
aliwasilisha kesi katika mahakama kuu kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
Odinga anasisitiza
kuwa aliibiwa ushindi wake katika kile ambacho kimewaudhi washirika wa kisiasa
wa Rais Kenyatta ambao wamekuwa wakimtaka akubali alishindwa.
Chanzo BBC
Chanzo BBC
0 Response to "RAILA ODINGA ADAI UCHAGUZI WA 2013 JESHI LILISHIRIKI KUMDHULUMU"
Post a Comment