![]() |
Mh.Said
Ramadhani Bwanamdogo enzi za uhai wake.
|
KIlichomuua Mbunge wa Chalinze Mh. Said
Bwanamdogo kinajulikana kwamba ni ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu na
habari za kulazwa kwake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi
zilianza kuwa hewani takriban wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo taarifa zaidi za ni ugonjwa
gani huo uliokuwa ukimsumbua bado hazijawekwa hadharani, huku Bunge chini ya
Spika Mama Anna Makinda likiendelea na maandalizi ya mazishi ya Mbunge huyo
aliyefariki leo asubuhi Jumatano ya tarehe 22/1/2014 .
Awali ilikuwa imeelezwa kwamba Mbunge
huyo alikuwa mahututi Moi na taratibu za
kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi zilikuwa zikifanywa. Baadhi ya wabunge
wenzake kutoka Mkoa wa Pwani akiwemo, Dr Seif Rashid wa Rufiji na naibu waziri wa afya
pamoja na Mh Koka mbunge wa Kibaha mjini walimtembelea hospitalini hapo
hivi karibuni.
Poleni wananchi wote wa Jimbo la
Chalinze na Watanzania kwa ujumla na Mwenyezi Mungu ailaze Pema Peponi Roho ya Marehemu
AMINA.
0 Response to "UGONJWA ULIOMUUA MBUNGE WA CHALINZE MH. 'SAID BWANAMDOGO' "
Post a Comment