MAKALA NA BLOGU YA MAISHA NA MAFANIKIO
Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi
wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza
kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako.
Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na
maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano
inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni
mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula
cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka
kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu
bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu
anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika
kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki
ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia
tofauti……!) Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa
tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni
kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo
lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako.
Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe
wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume
wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume
wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu
kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa
chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki
utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1.
Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibuna kutumia muda
mwingi kuwa naye
2.
Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsiatakavyo vutiwa na
mavazi yako pale atakapokuona
3.
Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako
au mumeo
4.
Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka
ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi
5.
Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale
unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka
au ushauri
6.
Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye
wa kimapenzi au ndoa
7.
Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au
inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8.
Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi
wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa
ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi
kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue
uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
Habari/mada hii nimetumiwa na
mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi
nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengi wafaidike
na ELIMU hii.
0 Response to "WANAWAKE NA HISIA ZA USALITI: ZIJUE DALILI ZAKE!!"
Post a Comment