Imedaiwa
kwamba mrembo, muigizaji nyota nchini Tanzania Wema Sepetu ameanzisha taasisi,
ya kitapeli inayojihusisha na utoaji mikopo.Taasisi hiyo kwa jina ‘Saving
Foundation Loans’, tayari imelalamikiwa na watu kadhaa kwamba imeshawaingiza
mjini kwa kuwaahidi kuwapa mikopo ndani ya dakika 45 lakini ikadhihirika kuwa
ni kinyume chake baada ya wahusika kuona kimya hata pale walipokamilisha
taratibu zote ikiwa ni pamoja na kujaza fomu kwenye mtandao pamoja na kutuma
kiasi cha fedha kupitia mitandao ya namba za simu walizoziweka hapo kwenye
tovuti yao.
Akizungumza
na Wapo Radio FM kupitia kipindi chake maarufu cha Patapata mmoja wa wahanga
hao alisema kwamba tayari amekwisha fikisha taarifa hizo polisi na wameahidi
kulifuatilia suala hilo kupitia kitengo chake cha kuzuia uhalifu wa kwenye
mitandao “Cyber crime investigation”. WAPO Fm ilipofanya jitihada za kutaka
kupata ukweli ikiwa kama kweli mkurugenzi wa taasisi hiyo ni huyu huyu Wema
Sepetu tunayemfahamu hatimaye ilibaini ya kwamba siyo kweli, matapeli hao kwa
kumtumia msichana aliyeigiza sauti kama ya Wema ndiye anayepokea simu na
kujitambulisha kwa wasiwasi kuwa ni Wema Sepetu.
Hata
namba wanayoitumia nayo imesajiliwa kwa jina la Wema Sepetu. Mwandishi
alipombana kwa maswali aeleze ofisi zilipo na iwapo angeweza kuonana naye ana
kwa ana Wema sepetu huyo feki alibabaisha babaisha na kusema “Usinichoshe na
maswali” akakata simu na kuingia mitini.
Wapo
haikuishia hapo ikamtwangia Wema Sepetu Original, Wema alikana kuhusika na
kampuni hiyo akasema kwanza yeye hata kwenye face book yenyewe tangu mwaka jana
amesitisha kwa hivyo mtu yeyote asijetapeliwa huko kwa imani kuwa kampuni ni ya
Wema sepetu, amewaasa watu kuwafikisha katika vyombo vya sheria matapeli hao
wanaotumia jina lake kutaka kujitajirisha bila jasho.
0 Response to "‘WEMA SEPETU’ AFUNGUA KAMPUNI YA KITAPELI DAR KUJIPATIA MAMILIONI YA PESA."
Post a Comment