Aliko Dangote |
Bilionea anayeongoza kwa
utajiri Barani Afrika, Aliko Dangote ameiambia BBC kwamba wajasiriamali kote
Barani Afrika wanapaswa kuweka mipango ya kukopa fedha ili kuendeleza biashara
na miradi mbalimbali wanayoianzisha. Amezitaka pia serikali kuacha kutegemea uwekezaji
kutoka nje.
Akielezea jinsi alivyoanza
biashara hapo mwaka 1978, alisema kuwa fedha za mtaji ‘SEED MONEY” alizipata
kutoka kwa marehemu babu yake kiasi cha Naira elfu tano za Kinaijeria baada ya
kuingia jijini Logos kujaribu kutafuta biashara ya kufanya.
Alisema biashara
ilichanganya harakaharaka kinyume na
matarajio yake kiasi kwamba baada tu ya miezi 6 tu aliweza kurejesha kiasi
chote cha fedha alizokopeshwa na babu yake. Alianza na biashara ya kuagiza bidhaa
chache kwanza ambazo zilikuwa ni sukari, mchele na samaki wabichi hapo mwaka 1980 na baada ya hapo mtaji uliendelea
kukua na kukua zaidi.
Alipoulizwa ni kwa nini
hakuingia kwenye biashara ya mafuta wakati huo ambapo ilikuwa inasadikika kuwa
ndiyo yenye kutajirisha haraka alisema kwamba, kwa bahati mbaya watu hudhania
hivyo lakini kumbe sivyo na yeye binafsi amelithibitisha hilo kwa kutajirika na
kuwa mtu tajiri zaidi Barani Afrika kupitia biashara isiyokuwa ya mafuta.
“Mafuta nadhani humfanya mtu
kuwa mvivu” Alimalizia Bilionea huyo
mwenye pesa nyingi kushinda matajiri wengine wote barani Afrika.
Msikilize Dangote mwenyewe hapa chini akizungumza ;
Ilike the message from Aliko Dangote that we entrepreneurs must borrow to increase investment regime
ReplyDelete