Gonjwa hatari la Dengue watu wamelifananisha na Tauni au
hata Ukoma zama za Yesu Kristo, kutokana na jinsi ambavyo hauna dawa wala kinga
inayoaminika zaidi ya kujikinga na mbu wanaoeneza ugonjwa huo waitwao Aedes.
Katika zama hizo za Masihi Yesu Kristo magonjwa hatari kama Tauni na ukoma yalikuwa yanaogopewa sana hata kufikia hatua ya watu kuwatenga wale waliokuwa wakikumbwa na magonjwa hayo. Watu walikuwa na imani potofu kwamba ukikaa karibu na mgonjwa wa aina hiyo basi ungeweza kuambukizwa. Hawakuwa na elimu kama ilivyokuwa sasa hivi kwamba magonjwa mengi yalienezwa na wadudu kama mbu au panya.
Tofauti na kipindi hicho sasa hivi maendeleo ya sayansi
na teknolojia yamewezesha binadamu kubaini vyanzo vya magonjwa mbalimbali, kwa
mfano gonjwa kama hili la Dengue linalowatesa wakazi wa jii la Dar es salaam na
haijulikani kama litafika mikoani au la, inajulikana wazi kabisa kuwa mtu
hawezi akaambukizwa kupitia mwenzake anayeumwa aidha kwa kugusana au hata kwa
kushirikiana chakula.
Lakini kuna jambo moja nimeligundua, kama ugonjwa
utazuka eneo fulani basi uwezekanao wa watu waliokuwa pale karibu nao kupatwa
na ugonjwa huo unakuwa mkubwa sana. Madhalani tunasikia kutoka taarifa
mbalimbali kwamba maeneo kama vile katika mahospitali watu wengi zaidi
wamepatwa na maambukizi ya dengue wakiwemo wahudumu wa hospitali na wakati
mwingine hata madaktari.
Sababu kubwa inaweza kuwa ni kutokana na hao mbu kuwauma
waathirika na kisha kwenda kuwauma wasioathirika na kwa kuwa wagojwa wengi
hukimbilia mahospitalini pindi tu wanapoumwa basi hiyo ndiyo sabau kubwa na
wala siyo kwamba wahudumu hao huambukizwa wanapowahudumia wagonjwa kama ambavyo
watu wengi wangeweza wakadhania. Na ukizingatia mazingira ya hosp[itali zetu
nyingi jijini yalivyokuwa rafiki wa mazalia ya mbu nayo huchangia kwa kiasi
kikubwa.
Historia inatuambia hata Ugonjwa wa malaria nao kabla
haujajulikana mti wa Quinine na Mapadri wa shirika la Majesuite huko Peru
America ya kusini baada ya kutambulishwa na wenyeji wa huko waliokuwa
wakiutumia kwa miaka mingi, watu wengi barani Ulaya waliteseka sana na kufa
huku wakijiona hivihivi kwa ugonjwa uliodhaniwa kusababishwa na mazingira yenye
majimaji, watu hawakujua kumbe homa ile ilienezwa na mbu ambao nao walipendelea
kukaa maeneo hayo ya umajimaji.
Kisa mpaka mapadiri hao kuja kugundua mti wa quinine
kuwa unatibu malaria na kuusambaza maeneo mengine yote ya ulaya, pale hata Mapapa wa Kanisa nao walipopatwa na homa hiyo kali ya Malaria na kupoteza maisha. Ilibidi ‘wasomi’
hao wanaoaminika kuwa na akili nyingi kujitahidi kuitangaza dawa hiyo Roma na ulaya nzima ambapo mpaka leo hii ndiyo tiba
kuu ya malaria ukiachana na ule mti mwingine maarufu wa kichina, ‘Artemisinine’.
'Ades' mbu aenezae Dengue |
Kama ilivyokuwa Malaria kwamba haikuchagua ni nani
aumwe, hata Mapapa watu waliosadikiwa kuwa watakatifu nao waliupata ndivyo
hivyo hivyo na Dengue leo hii inavyofanya. Tumesikia Madaktari kuugua na hata
kufa, wasanii wakubwa na si ajabu hata ukasikia viongozi wakubwa tu serikalini
na katika taasisi mbalimbali nao wakipatwa na gonjwa hili hatari. Halichagui
masikini, tajiri, kiongozi wala mtu wa kawaida, wote wanauwezekano wa
kuambukizwa ili mradi tu awe ni binadamu.
SULUHISHO LA DENGUE
Chakufanya sasa wanajamii killa mmoja na nafasi yake
tuchukue hatua, leo hatuna shida ya kufahamu ni kitu gani kinasababisha Dengue,
hebu kila mtu ahakikishe mazingira yanayomzunguka iwe ni nyumbani kazini au
hata kwenye mashule na taasisi zote, yanakuwa safi tuondoe mazalia ya mbu na
hata ikiwezekana tusione hasara kutoa sh. Elfu mbili, tatu, hata tano kununua
viua-wadudu tukanyunyizia maeneo yanayotuzunguka.
Tunaweza hata kujikuta tukiua ndege wawili kwa jiwe moja
kwani kwa kufanya hivyo tutajikuta hata na malaria nayo tukiipunguza kwa kiasi
kikubwa sana. Tumeshazoea tukipatwa na malaria tunakimbilia dukani kununua
mseto au SP, siku mbili, tatu tumepona, ndugu yangu Dengue ni tofauti, ni
ugonjwa wa virusi kama ukimwi ila tofauti yake tu ni kwamba virusi hivi huweza
kutoweka vyenyewe kama vile vya mafua baada ya siku chache. Lakini wakati
mwingine pia huweza kuua.
Serikali nayo ichukue hatua za makusudi mithili ya inavyofanya wakati wa ujio wa viongozi wa kigeni mfano walivyokuja Clinton, Bush na Obama. Hakuna mtu ambaye hakushuhudia kampeni ya usafi wa hali ya juu ulivyofanyika kwa kila hali hadi barabara zikafyagiliwa mpaka usiku wa manane, iache visingizio kibao kwamba Dar ina madimbwi ya maji huku ikikaa kimya watu tukiteketea kwa Dengue.
Msikilize Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hapa Said Mec Sadik akisisitiza hatua za kuchukua ili kukabiliana na ugonjwa huo;
Serikali nayo ichukue hatua za makusudi mithili ya inavyofanya wakati wa ujio wa viongozi wa kigeni mfano walivyokuja Clinton, Bush na Obama. Hakuna mtu ambaye hakushuhudia kampeni ya usafi wa hali ya juu ulivyofanyika kwa kila hali hadi barabara zikafyagiliwa mpaka usiku wa manane, iache visingizio kibao kwamba Dar ina madimbwi ya maji huku ikikaa kimya watu tukiteketea kwa Dengue.
Msikilize Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hapa Said Mec Sadik akisisitiza hatua za kuchukua ili kukabiliana na ugonjwa huo;
0 Response to "DENGUE NI KAMA TAUNI NA UKOMA ZAMA ZA YESU KRISTO, UKIUPATA HAMNA DAWA"
Post a Comment