![]() |
Diamond Platnumz . |
….Nimetembea
tembea Bara na visiwani, ila nikajionea….Natamani nikupe ..hela sinaaa…Nimejaliwa
pendo, heshimaa ….Wana wivu hao, haoo… hao, wachonganishi hao, haoo hao….Usijeniacha kwa unyonge,
nitachechemea ….
……Mwendawazimu
kaingiaje… Kitomondo kitomondo… mwendawazimu kaingiaje……
,,,,,,,KITOMOMDO…….KITOMONDO……
…WANA
WIVU HAO..HAOOO… HAO….
Hivyo
ni baadhi tu ya vionjo vilivyopo ndani ya mashairi ‘lyrics’ ya ‘songi’ hili kali “KITOMONDO” la mkali Diamond
Platnumz linalotarajiwa kutoka rasmi hivi karibuni, kwani hii ‘version’ siyo
halisi hata ukisikiliza tu sauti yake (ubora) siyo wenyewe original, ni wajanja
tu kama ujuavyo Bongo yetu, wameamua kuvujisha kitu kabla hata mwenyewe Diamond
hajakiweka hadharani ‘oficially’.
Kwa
kweli siyo jambo zuri kabisa hata kidogo, hali hii inarudisha sana nyuma
maendeleo ya muziki na wajasiriamali wanaotaka kutoka kupitia fani hii. Ingefaa
sana serikali kupitia sheria zake ikakaza zaidi ile sheria ya haki miliki ya
kazi za ubunifu na sanaa ili hapo baadaye kuondoa kabisa ujanja ujanja huu
ambao katika nchi za wenzetu hata kama upo siyo kwa kiasi cha kutisha kama
ilivyokuwa hapa kwetu Tanzania.
0 Response to "MUZIKI MPYA MKALI 'KITORONDO' WA DIAMOND NI GUMZO LA JIJI: UDOWNLOAD HAPA"
Post a Comment