Habari kutoka katika eneo hilo
zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo
yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji
cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.
Diwani wa Samunge, Jackson
Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika
kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.
“Hadi sasa kuna watu zaidi ya
4,000 na bado wanaongezeka, hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu
wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na
kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba,” alisema Sandea.
Alisema tofauti na maeneo
mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la
mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.
“Kuna wengine wanapata hata
mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi,” alisema.
Ulinzi
waimarishwa
Diwani huyo alisema ulinzi
umeanza kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo,
kunaweza kutokea vurugu kubwa na hata mauaji.
“Sisi kama viongozi, tumeweka
utaratibu mzuri wa kuchimba madini kiusalama na hata wale ambao wameanza kuuza
mashamba yao, tunawawekea utaratibu mzuri,” alisema.
Maofisa
madini kutua Samunge
Kamishna wa Madini Kanda ya
Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za
kugundulika kwa dhahabu katika eneo la Samunge, maofisa wake wanajiandaa kwenda
kijijini hapo.
'Pande la dhahabu ghafi’ |
Alisema taarifa za kitaalamu
kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo Samunge itatolewa baada ya maofisa hao
kufika katika eneo hilo na kufanya utafiti.
Ahadi
ya Babu
Kugundulika dhahabu katika
eneo hilo kunahusishwa na ahadi ya Mchungaji Mwasapila kuwa mamilioni ya watu
watafika tena Samunge baada ya kupungua ikilinganishwa na miezi ya mwanzo baada
ya kuanza kutoa tiba ya kikombe cha dawa iliyodaiwa kutibu magonjwa sugu.
Tiba yake hiyo ambayo ilizua
utata kitaalamu na ikielezwa kuwa waliotibiwa waliugua tena na wengine
kupoteza maisha, aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema watu kutoka
mataifa yote watakwenda tena Samunge siyo kupata kikombe pekee, bali huduma
nyingine.
Licha ya wengi kuitilia shaka
kauli yake hiyo, aliendelea kuisisitiza na akikata miti na kujenga kituo
kikubwa cha kutolea huduma ya kikombe.
HABARI NA MWANANCHI.
0 Response to "SAMUNGE KWA BABU MAFURIKO UPYAAA, SAFARI HII SIYO KIKOMBE BALI NI DHAHABU."
Post a Comment