![]() |
Bendera ya Tanzania |
Kiashiria kingine cha utovu wa kufikiri kwa Watanzania
kinadhihirika katika mambo kama vile, upinzani mkali kwa wale watu wanaojaribu
kuibua masuluhisho kwa matatizo mbalimbali hususani umasikini na magonjwa.
Mfano mzuri tunauona kwa Askofu Sylvester Gamanywa na kampeni yake ya
kuwamilikisha vijana uchumi.
Wamediriki kujitokeza watu tena wenye dhima kubwa tu
katika jamii waliodiriki kuonyesha upinzani wa ajabu kwa kudai eti yeye
Gamanywa ameingiza biashara kanisani, tena biashara za ‘Kishirikina”,
wamemhusisha na vyama/taasisi zisizoeleweka. Huo ni uvivu mkubwa wa kufikiri,
mtu kujaribu kumsingizia mwenzake mambo yasiyoeleweka ilihali mtu huyo
anachofanya ni jambo la kheri lenye lengo la kuwakomboa watu kutokana na
umasikini.
Inawezekana pia kuwa ni wivu tu, mtu anaona anachofanya
mwenzake ni kitu kizuri, sasa ili na yeye aonekane au kusikika, basi anajaribu
kuponda. Gamanywa inafaa apewe moyo, na siyo yeye tu, mtu yeyote anayejaribu
kuleta suluhisho la kweli la umasikini haipaswi tumkatishe tamaa, haijalishi ni
wa dini gani, awe mkristo awe Muislamu, awe Mhindi, tusiangalie dini wala
kabila bali tuangalie tutaondokaje pale tulipo.
Watanzania tuache imani potofu za aina yeyote ile
zinazolenga kuturudisha nyuma kimaendeleo, suluhisho la matatizo yetu mengi ni
kuutokomeza umasikini na umasikini hauwezi ukaondolewa kwa ushirikina, hila
wala imani potofu, bali ni kwa kufanya kazi kwa bidii huku tukifuata kanuni
bora za kisayansi zilizothibitika na
zilizoweza hata kuwatoa na kuwakomboa
Wamarekani, Wachina, na Mataifa yote yaliyopiga hatua kimaendeleo.
Hebu sikiliza kidogo audio hizi zinazohusu BCIC na kampeni nzima ya Askofu Sylvester Gamanywa juu ya kuwarithisha vijana ili waweze kuondokana na umasikini wa kipato.
Hebu sikiliza kidogo audio hizi zinazohusu BCIC na kampeni nzima ya Askofu Sylvester Gamanywa juu ya kuwarithisha vijana ili waweze kuondokana na umasikini wa kipato.
0 Response to "UWEZO WETU WA KUFIKIRI WATANZANIA NI MDOGO:TAFITI"
Post a Comment