VITABU HUBADILISHA MAISHA YA WATU WENGI: ‘THINK BIG’ | JIFUNZE UJASIRIAMALI

VITABU HUBADILISHA MAISHA YA WATU WENGI: ‘THINK BIG’

Paul Mashauri Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na makongamano ya kuelimisha ujasiriamali kwa njia ya kuongea EASB group akiongea na wanachuo wa chuo cha Ustawi wa jamii jijini Dar es salaam.

Katika ‘speech’ hiyo nzuri alikuwa akiwatia moyo vijana kuwa waamini wanao uwezo mkubwa ndani yao kuliko wanavyofikiria. Akitolea mifano ya watu waliofanya mambo makubwa Duniani wakiwa vijana, aliwataja Yesu Kristo, Mtume Muhamad, Bill Gates na Mark Zuckerberg.

Pia akitoboa siri ya mafanikio yake aliyoyapata ndani ya kipindi kifupi tangu amalize chuo kikuu Mlimani alitaja ni  Kitabu kimoja kiitwacho THINK BIG alichopewa zawadi na mama mmoja wa jirani, anasema baada tu ya kukisoma kitabu hicho kiliyabadilisha maisha yake kabisa mpaka sasa anapotoa ushuhuda huu.


Think Big ni moja ya vitabu maarufu sana duniani, kimeandikwa na mwandisi Mmarekani Ben Carso. Kinaelezea mafanikio ya mwandishi huyu mwenyewe binafsi aliyelelewa na mama yake pekee huku akichekwa na watu wakiwemo hata na waalimu wake. 

Lakini kutokana na kutiwa moyo na mama yake alikuja kuwa mtu mkubwa sana, Daktari wa kwanza Duniani kufanya operesheni ya kuwatenganisha mapacha walioungana vichwa.

0 Response to "VITABU HUBADILISHA MAISHA YA WATU WENGI: ‘THINK BIG’"

Post a Comment