Diamond Platmumz akifanya mahojiano leo hii usiku na kituo cha redio cha Times Fm amesema kwamba yeye wakati alipokuwa akienda kufanya collabo (ushirikiano) ile nyimbo ya “My number one” hakuwa anafahamika Kimataifa. “Watu waliongea mengi sana lakini lakini hawakujua fikra zangu zilikuwa nini, lakini ile nyimbo ndiyo iliyopita na kuniingiza MTV….ile nyimbo……”
![]() |
DIAMOND PLATNUMZ |
Kuhuiana na madai
kuwa anaringa kadiri anavyopata mafanikio alikanusha na kusema kuwa yeye
amekuwa akiwasaisia watu wengi tu na wale wanaompaka matope ni wachache ambao
wanajidai wanamjua sana na kutaka ‘kumcontrol’. Amesema hadi leo hii anatenga
muda na hata kukiwa na shughuli mbalimbali kama msiba au sherehe mitaa yake ya
zamani uswahilini Tandale bado huwa anakwenda kujichanganya na watu na wala
hawafanyii unyanyapaa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Zaidi ya yote MKALI Diamond
ametanabahisha kwamba “mission” yake kubwa ni kuimba katika lugha ya kiingereza
kwa baadhi ya nyimbo zake kwani moja ya sababu zilizomkosesha tuzo ni pamoja na
kutokuimba katika lugha inayojulikana kimataifa, alisema wasanii wa kinaigeria
wana advantage kubwa kwa kuimba kwa kiingereza lakini pia akasema siyo lazima
sana kuimba katika lugha ya kiingereza ili kufanikiwa kwani midundo nayo ni
kigezo, mfano kuna wasanii Nigeria japo hawaimbi kwa kiingereza lkakini kwa kuwa nyimb zao zinachezeka basi
wameweza kupata tuzo. Lakini anadai Watanzania wanapenda zaidi miziki yenye
hadithi za kimapenzi, “fulani kamuacha fulani, ukienda kuimba ukilalamika
mapenzi huko nje watu hawatakuelewa kabsa, wanataka muziki unaochezeka”
Msikilize mwenyewe Diamond hapa chini akifanya mahojiano na Kituocha redio cha TIMES FM.
Msikilize mwenyewe Diamond hapa chini akifanya mahojiano na Kituocha redio cha TIMES FM.
0 Response to "DIAMOND PLATNUMZ:KABLA SIJAFANYA COLLABO NA DAVIDO NYIMBO ZANGU ZILIKUWA MWISHO CHALINZE "
Post a Comment