Waathirika wa moto ulioteketeza soko la wafanyabiashara wadogo, maarufu kama soko la mchikichini au soko la Karume wamelalamika kuwa huenda zikawa ni njama zilizosababisha kuungua kwa soko hilo kwani hata mamlaka zinazohusika ikiwemo zima moto hawakuonekana kufanya jitihada za kutosha wakati moto huo ulipozuka jana tarehe 11 majira ya saa nne na nusu usiku.
Jifunzeujasiriamali
ilitembelea eneo la tukio leo majira ya
saa 10 jioni na kujionea hali halisi ilivyokuwa ambapo mpaka wakati huo bado
moto ulikuwa ungali ukiwaka katika baadhi ya maeneo hasa yale yaliyokuwa maalumu
kwa biashara za viatu. Mfanyabiashara mmoja anayefanya shughuli za kuhifadhi
mizigo ya wafanyabiashara kwa jina moja la Costa, alisema kwamba muda huo wa
saa nne usiku alishuhudia moto huo ukianzia maeneo ya katikati karibu na yalipo
mabanda ya mamantilie akafikiri moto ule ungedhibitiwa tu lakini kadiri muda
ulivyopita ukazidi kusambaa.
Anasema cha ajabu
moto ule ulimshangaza kwani ulisambaa haraka sana katika staili ambayo utadhani
kuna mtu alikuwa akiufukiza chini kwa chini kuelekea kulikokuwa na mabanda ya
nguo na viatu. Costa anaendelea kusema kuwa Gari la faya lilipofika waliingiwa
na matumaini wakidhani sasa moto ungedhibitiwa lakini walishangaa kusikia eti
gari la faya lisingeweza kupenya katikati ya vibanda kutokana na kutokuwa na
barabara pana.” Kwa nini hata wasingelilazimisha hata kuharibu baadhi ya mabanda
ilimradi tu gari limepenya katikati” anauliza Costa kwa hasira.
Waliishia kuzima kandokando ya soko tu kuzuia moto usishike nyumba za jirani na
upande wa kiwanda cha bia Tanzania Breweries.
![]() |
SOKO LA WAMACHINGA MCHIKICHINI LIKITEKETEA KWA MOTO |
Costa anasema
walijitahidi kuokoa baadhi ya mali zisiteketee lakini tatizo lilikuwa vibaka
nao kuwaibia pindi walipokuwa wakienda kurudia kutoa mali zingine, anasema
polisi nao walikuwa wakiwakataza kuokoa mali kwa hofu ya kupoteza maisha au
kupata majeraha ya moto.
Watu wengi walisikika wakikumbuka suala la bima huku wengine wakihoji ikiwa hata wafanyabiashara wadogowadogo kama wamachinga wanaweza kujiwekea bima kama ilivyokuwa kwa biashara kubwa.
Watu wengi walisikika wakikumbuka suala la bima huku wengine wakihoji ikiwa hata wafanyabiashara wadogowadogo kama wamachinga wanaweza kujiwekea bima kama ilivyokuwa kwa biashara kubwa.
Nyakati za mchana
walionekana watu mbalimbali wakiondoa baadhi ya mabaki ya mabanda yao
yaliyoungua huku wengine ambao inasemekana wala siyo waathiriwa wakijikatia
mabomba ya nguzo za chuma bila wasiwasi wowote, utathani ni wahusika vile.
Inasemekana mabomba hayo huenda kuyauza kama chuma chakavu.
Hata hivyo mamlaka
zinazohusika jijini Dares salaam likiwemo jeshi la polisi zimekwishatoa tamko
leo jioni wakiwataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu huku uchunguzi kamili
ukifanyika kubaini chanzo halisi cha moto huo, na ikiwa kulikuwa na hujuma za
aina yeyote ile kutoka kwa taasisi au mtu yeyote yule.
0 Response to "HUJUMA ZATAJWA KUUNGUA SOKO LA WAMACHINGA MCHIKICHINI/KARUME"
Post a Comment