Aklisoma bajeti ya mwaka
2014/2015 Bungeni, Waziri wa fedha Saada Mkuya Salum amesema kwamba misamaha
mbalimbali ya kodi ikiwemo msamaha wa kodi kwa makampuni ya michezo ya
kubahatisha pamoja kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa ndege kwa walipakodi
wasio wakazi yaani non resident na hatua hii inalenga katika kupunguza misamaha
ya kodi na hivyo kuiongezea mapato serikali.
Aidha waziri wa fedha alisema kwamba, serikali itatoa unafuu kwa wafanyakazi
kwa kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira 'payee'
kutoka asilimia 13% ya sasa hadi asilimia 12% na amesema serikali itaendelea
kuangalia uwezekano wa kuendelea kupunguza kiwngo hiki hatua kwa hatua ili
kuwapa nafuu wafanyakazi.
 |
WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM |
Kwa upande wa wafanyabiashara wadogo wadogo wanaozidi mauzo ya shilingi milioni
nne kwa mwaka lakini wasiozidi milioni 7 na nusu kwa mwaka kiwango cha kutozwa
kodi kwenye mapato hasi kimeongezwa kutoka asilimia 2% hadi asilimia 4% kwa
wale wanaoweka kumbukumbu za mauzo na kutoka sh. laki moja hadi sh. laki 2 kwa
wale wasiokuwa na kumbukumbu za mauzo. Lengo lake ni kuongeza mapato ya
serikali kwa shilingi bilioni 31 na mia tano na nne.
Msikilize
‘live’ waziri wa fedha Mheshimiwa Bi Saada Mkuya Salum akisoma bajeti hiyo
ya serikali kwa mwaka 2014/2015 Bungeni mjini Dodoma leo.
0 Response to "MISAMAHA YA KODI YAFUTWA NA WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM "
Post a Comment