CHOMBO KILICHOTUA JUU YA KIMONDO , UNAJIFUNZA NINI MJASIRIAMALI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHOMBO KILICHOTUA JUU YA KIMONDO , UNAJIFUNZA NINI MJASIRIAMALI?


Muonekano wa kimondo 'comet67'
wakati chombo kikitaka kutua.
Miaka 25 tangu wazo la kukituma chombo hiki lilipoasisiwa, miaka kumi ya chombo kusafiri angani takribani kilomita nusu bilioni, na sasa leo hii, hatimaye chombo ‘Philae’ kimefanikiwa kutua salama juu ya “KIMONDO” ("Comet67p/Churyumov-Gerasimenko"), jiwe kubwa lenye upana wa kilomita 4, ambalo linashabihiana na dunia yetu hii kwa kuwa na vumbi na miamba iliyokaa kama milima na linalosadikiwa kutoa majibu mengi ya jinsi ulimwengu ulivyoanza miaka zaidi ya Bilioni 4.5 iliyopita.

Kimondo hiki kinakadiriwa kuwa na umri zaidi ya  ya miaka bilioni 4 sawa na dunia yetu, kina uzito upatao  tani bilioni 10, na huzunguka angani kwa kasi ya kilometa 18 kwa sekunde moja.

Inasadikiwa  na wanasayansi kuwa Vimondo  huenda ndivyo vilivyohusika na kuleta maji katika dunia yetu hii pamoja na viasili vilivyohusika katika kuanzisha uhai na viumbe hai vilivyokuwepo Duniani tukiwemo na sisi binadamu. Chombo hiki kimetumwa na wanasayansi kutoka Ulaya na hii ndio misheni yao iliyopata mafanikio makubwa zaidi ukilinganisha na mishenizilizowahi kufanywa na wanasayansu kutoka Marekani, Urusi, China na India.

Eneo kilipotua kimondo "PHILAE"
Jambo moja kuu ambalo kama wajasiriamali tunalopaswa kujifunza ni uvumilivu na kutokukata tamaa.Hebu fikiria jambo hilo lilifikiriwa tangu miaka zaidi ya 25 iliyopita, likaja kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10, chombo kikisafiri angani, hadi leo hii kilipotua na kuanza kutuma picha duniani. Sisi tunaanzisha biashara au mradi, hata kabla miaka miwili haijapita tunakata tamaa na kutafuta shughuli nyigine ya kufanya, hatuvumilii, matokeo yake tunabakia bila ya kuwa na jambo kubwa la kutimiza katika maisha yetu.


0 Response to "CHOMBO KILICHOTUA JUU YA KIMONDO , UNAJIFUNZA NINI MJASIRIAMALI?"

Post a Comment