Kwa mujibu wa Jarida la Marekani la Forbes lililotoka
mwishoni mwa mwaka huu, Mfanya biashara maarufu
nchini, Rostam Aziz(50) ndiye tajiri anayeshilkilia nafasi ya kwanza kwa
sasa hivi nchini Tanzania. Taarifa hizo zilianza kutoka juzi.
Rostam alishika nafasi hiyo huku katika matajiri wa
Afrika nzima akishikilia nafasi ya 27
akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani bilioni moja sawa na
Shilingi za Kitanzania trilioni 1.6 Hii
ni mara yake ya tatu Mbunge huyo wa Igunga kuingia katika orodha ya matajiri 50
wa Afrika tangu mwaka 2011 aliposhika nafasi ya pili baada ya Said Salim
Bakhres kuwa namba 1. Dr. Reginald Mengi alikuwa wa tatu akifuatiwa na Ali
Mafuruki. Mwaka jana pia Rostam Aziz kulingana na jarida hilohilo alishikilia
nafasi hii hii aliyoshika mwaka huu.
ROSTAM
AZIZ ‘BILIONEA NUMBER ONE IN TANZANIA’
|
Aliyekamata nafasi ya pili mwaka huu ni Mbunge wa Singida
mjini Mohamed Dewji au ‘MO’. Mo safari
hii amempiku Reginald Mengi kwa kuwa katika nafasi ya pili Tanzania huku
akishika nafasi ya 31 Afrika nzima kwa utajiri wa Dolla za Kimarekani milioni
800, mwaka jana Dewji alikuwa sawa na Bakhresa kwa kushika namba 3, Tanzania Na
namba 38 Afrika wote wakiwa na utajiri wa Dola nusu Bilioni sawa na shilingi za
Kitanzania Bilioni 783.
Rostam Aziz kwa mara ya kwanza kabisa anaingia katika
orodha ya Mabilionea wa Dunia kwa kumiliki utajiri wa Dola bilioni moja na
zaidi.
Bakhresa mwaka huu anashikilia nafasi ya tatu Tanzania
wakati katika Bara la Afrika yupo namba 44 kwa utajiri wa dola za kimarekani
milioni 575. Mzee Reginald Mengi ameshikilia nafasi ya 4 kwa Tanzania, huku
katika Bara la Afrika akishika namba 45 akiwa na utajiri wa Dola za Kimarekani zipatazo milioni 560.
Jarida hilo la Forbes linaripoti kuwa Utajiri wa Rostam
Aziz umetokana na biashara ya
mawasiliano hasa ya simu za mkononi ya Vodacom ambapo anamiliki hisa asilimia
35%.Vvilevile anamiliki biashara za uchimbaji wa madini na ujenzi.
Katika Afrika tajiri namba moja ni Aliko Dangote
aliyeshika nafasi hiyo kwa muda mrefu sasa, akifuatiwa na familia ya Johanny
Ruppet wa Afrika ya Kusini, wa tatu ni Nick Oppenheimer wa Afrika ya Kusini pia.
Wa nne ni mwanamke mtoto wa rais wa Angola, Isabel Dos Sntos ambaye pia ndiye mwanamke
tajiri kuliko wote katika Bara la Afrika.
Wiki mbiuli zilizopita taarifa kutoka kartika jarida
jingine liitwalo Ventures Afrika
lilitoka na matokeo ya utafiti wake uliosema kwamba Bilionea namba moja
Tanzania ni Mohamed Dewji akifuatiwa na Rostam Azizi.Deji pia alitajwa kuwa
bilionea kijana zaidi Barani Afrika akimiliki utajiri wa Dola za Kimarekani
Bilioni 2 sawa na sh. trilioni 3 za kitanzania klwa mujibu wa jarida hilo la ‘Ventures
Africa’
0 Response to "ROSTAM AZIZ BILIONEA TAJIRI NAMBA MOJA TANZANIA 2014, WA PILI NI MOHAMED DEWJI, ‘FORBES’"
Post a Comment