Mwanasayansi mashuhuri nchini Uingereza ‘Stephen Hawking’
ameonya kwamba juhudi zinazoendelea za kuunda ‘roboti’, mashine inayofikiria a
kutenda kama binadamu zinaweza zikasababisha maafa makubwa kwa kizazi cha
binadamu siku za usoni na kusababisha kutoweka kwake.
Stephen Hawking |
Alikuwa akijibu swali aliloulizwa juu ya mashine yake yenye
uwezo wa kujibu maswali kama binadamu na iliyotengenezwa kwa teknolojia msingi
katika kuunda binadamu huyo wa bandia mwenye uwezo sawa au hata kushinda ule wa
binadamu wa kawaida. Teknolojia hiyo tayari imekwishaanza kutumiwa kwa watu
waliokuwa na magonjwa yanayohusisha matatizo katika kuzungumza.
Alisema kuwa binadamu kamili wa bandia ataweza kuwa
ametengenezwa miongo michache ijayo kutoka sasa na hatua zilizokwisha pigwa
mpaka sasa zimethibitika kuwa na mafanikio makubwa, ila tu ni kwamba
haijajulikana dhahiri endapo binadamu huyo ikiwa atakuwa na akili kutuzidi
ataleta maafa makubwa kwa binadamu wa kawaida ama ataleta faida chanya.
Watu wengine wameanza kuingiwa na wasiwasi juu ya kazi
zinazofanywa na binadamu mahali pake kuchukuliwa na “wanadamu hao wapya” wenye akili
kupindukia.
Hata
katika sekta ya 'malavidavi' pia watatumika, ukimwi byebye!
|
Profesa Hawking pia alizungumzia faida na hasara za
matumizi ya mtandao wa Intaneti, akionya intaneti kugeuka kuwa kituo kikuu cha
Magaidi kutoa maelekezo ‘command centre for terrorists’. Alisema juhudi za
makusudi zinafaa zichukuliwe na makampuni ya intaneti kuzuia kitisho cha
magaidi hao lakini ugumu unabakia kuwa ni vipi itawezekana pasipo kuweka rehani
uhuru wa kujieleza pamoja na faragha.
chanzo bbc
0 Response to "HATARI! BINADAMU BANDIA WA KUTENGENEZWA KUCHUKUA MAHALI PA BINADAMU WA KAWAIDA"
Post a Comment