Ujasiriamali
ni nini hasa?
Katika
lugha ya Kiswahili
ujasiriamali unamaanisha, ujasiri
wa kutafuta mali. Lakini tukirudi nyuma
kidogo karne iliyopita kuangalia maana
aliyoitoa mwanauchumi raia wa Austria, “Joseph Schumpeter”;
Ujasiriamali maana yake ni Uratibu na Uendeshaji wa shughuli za
kibiashara kwa Ubunifu kwa lengo la kupata
Faida na utayari wa kukabilia na Hasara yeyote itakayojitokeza.
Tofauti iliyopokuwepo kati ya biashara na Ujasiriamali
Biashara ni nini?
Biashara ni shughuli yeyote ile halali anayoifanya mtu kwa lengo
la kupata faida, shughuli hiyo yaweza kuwa uuzaji wa bidhaa, utoaji huduma
au uzalishaji bidhaa.Ujasiliamali upo ndani ya biashara, “huwezi
kuwa mjasiliamali pasipo kuwa mfanyabiashara lakini unaweza ukawa mfanyibiashara
bila kuwa mjasiriamali”.
Umuhimu wa
Ujasiriamali.
Kimsingi kila mwanadamu hapa duniani ni
mfanyabiashara kutokana na ukweli kwamba shughuli zote azifanyazo mwanadamu
zinalenga kuleta faida lakini kati ya
hao wanadamu utakuta wapo maskini na matajiri. Kinachosababisha hali hiyo ni Ujasiriamali.
Kutokana na kila mtu kutamani afanikiwe
zaidi ya mwenzake hali ya ushindani hutokea (hali ya kila mtu kutaka
kuwafanyia wateja kitu cha ziada kitakachowanufaisha) na baadhi yao hufanya
mambo ya ziada ili kutimiza lengo hilo.
Mambo hayo au jambo la ziada ni lazima
liwe gumu na ambalo wakati mwingine
humhitaji mtu kulifanya kwa bahati na sibu pasipo kuwa na uhakika asilimia mia
moja kuwa atapata faida. Hali hiyo ndiyo huitwa ujasiriamali na siyo kila mtu
anaweza kufanya hivyo, ndiyo maana siyo kila mtu anayefanya biashara anaweza
akaitwa mjasiriamali.
Hata kabla ya wataalumu kugundua neno
ujasiriamali, ujasiriamali ulikuwepo tangu binadamu alipoanza kuishi duniani, tunaweza
tukasema ni tangu zama za mawe, wakati mababu zetu walipoanza kutengeneza moto
kwa kupekecha vijiti viwili huku wakiokoteza matunda, mbogamboga na mizizi
porini.
Hilo limedhihirishwa na maendeleo makubwa kuanzia zama hizo za kale za mawe mpaka leo hii zama
za ‘Intanet’. Bila shaka kuna baadhi ya
Binadamu waliokuwa wajasiriamali waliosababisha mabadiliko hayo ya
kiuchumi na kijamii kutokea.
Katika kundi la watu wengi, haiwezekani
wote wakawa wajasiriamali, ni lazima
wawepo wachache watakaoziona fursa za biashara na kuzitumia. Na hao ndio
huitwa wajasiriamali.
Katika nchi zilizopiga hatua kubwa katika
ujasiriamali, serikali zao zilihamasisha watu kupitia elimu mashuleni na vyuoni kama njia ya watu kujijengea
tabia za kijasiriamali ili baadaye waweze
kuingia katika dunia ya ushindani.
Tabia na uwezo wa
watu kuanzisha miradi inayolenga kuzalisha bidhaa na huduma mpya ambazo hazikuwepo awali inafaa ihimizwe.
Ubunifu
unatakiwa uwe ndiyo msingi wa ujasiriamali badala ya mazoea
ya kuanzisha miradi mipya bila
ya kuongeza vitu vitakavyoboresha
zaidi bidhaa /huduma husika. Vitu hivyo vitakavyoboresha bidhaa huduma
vyaweza kuwa bidhaa/huduma yenyewe, mfumo mpya wa masoko, mifumo mipya ya
usambazaji, njia mpya za uzalishaji, mifumo mipya ya kitaasisi nk.
Mfano mzuri ni bidhaa na teknolojia mpya
zinazoibuka kila siku na kuzifunika zile za zamani, hiyo yote ni kazi ya
wajasiriamali. Teknolojia kama ya Intaneti, barua pepe (e-mail) zimechukua mahali pa barua za kawaida na simu za mezani, ‘Player’
za santuri zinazotumia
umeme zilichukua nafasi ya ‘Gramaphones’ zilizozungushwa kwa mkono.
‘Radio cassettes’ zikachukua mahali
pa players. CD/DVD players
zikazipiku cassettes na sasa kuna vitu kama ‘MP3’ na ‘MP4’ players, Iphones, Smart Phones na simu za mikononi za aina kwa aina zenye
uwezo mkubwa wa kupiga muziki, kuonyesha picha na kuunganishwa na Intaneti.
Ujasiriamali ni kama uhai(pumzi)
inayosukuma uchumi wa soko huria. Makampuni makubwa hayawezi kuendelea kubakia
kileleni mwa soko milele ikiwa hayataheshimu kiini cha ujasiriamali ambacho ni
ubunifu. Ni lazima yakubali mabadiliko, yakubali kubomoa ‘yale mambo’ ya kizamani waliyoyazoea na kujenga mapya.
Kinachofanya Makampuni kama Johnson & Johnson,General
Motors, Microsoft, Apple na mengineyo kuendelea kufanya vizuri ni kuachana na
tabia za ukiritimba wa “kujifungia”, kutokuogopa mbadiliko, kuanzisha biashara
mpya na kufunga ama kuuza zile biashara za zamani ambazo zinaonekana
hazizalishi tena faida.
ASANTE SANA. 100%
ReplyDeleteAsante na wewe Muhidin
Delete