Uwakala wa makampuni ya simu za mkononi, kufanya miamala
ya kutuma na kupokea pesa hapa nchini Tanzania ni biashara inayokua kwa kasi kubwa na haijaanza siku nyingi. Ni kama miaka mitano
hivi hapa na 7 kwa wenzetu Wakenya ambako
ndiko huduma hii ilikozaliwa na baadae kusambaa katika mataifa ya Tanzania, Msumbiji,
Lethoso, Misri, Afrika ya Kusini, Afghanistan na Ulaya Mashariki.
Huduma hii ikiwa imeasisiwa na Vodacom chini ya Safaricom
na baadae makampuni mengine nayo kuanzisha , huduma zinazotolewa ni kama vile,
kuweka na kutoa pesa, kutuma pesa kwa watumiaji wengine wa mtandao na kwa wale
wasiotumia mtandao, kulipia bili mbalimbali kama maji, umeme nk. Kununua muda
wa maongezi na kuhamisha fedha kwenda
akaunti za mabenki au kinyume chake.
Kabla ya huduma hii kubuniwa, watumiaji wa simu za
mkononi walipata shida sana wakifikiria njia rahisi ambayo wangeweza
kuitumia katika kuwatumia wapendwa wao
pesa, wengi waliamua kutuma muda wa maongezi, na kisha anayetumiwa hulazimika
kwenda kuuza muda huo wa maongezi kwa watu wengine kama njia ya kupata kiasi cha fedha kilichotumwa. Ilikuwa ni njia
ngumu na iliyogharimu muda. Wataalamu wa Vodaphone baada ya kubaini tatizo hilo hapo mnamo mwaka
2007 wakaanzisha utafiti uliosababisha hatimae M- PESA kuzaliwa.
Tuachane sasa na historia hiyo ya m-pesa tuje moja kwa
moja kwenye mada yetu, miaka kabla ya 2012, jiji la Dar es salaam lilisheheni
vibanda vya kupigisha na kuchaji simu za mkononi, ambavyo wajasiriamali wengi
wadogowadogo walijiajiri kupitia hivyo. Lakini ujio wa huduma za kipesa kupitia
simu za mkononi umebadilisha kabisa sura ile na sasa katika kila kona ya jiji
utaona vibanda lakini vingi vikiwa vinatoa huduma za pesa za makampuni
mbalimbali yakiwamo Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Smart na TTCL.
Biashara hii ya kuwa wakala wa makampuni hayo ya simu
katika kufanya miamala ya pesa kwa wateja
mwanzoni ilionekana kama vile
siyo ‘dili’ nikiwa na maana kwamba haikuwa inalipa vizuri, hata ulikuwa ukienda
katika makampuni ya simu kuomba laini kwa ajili ya uwakala ulikuwa unapewa
chapchap. Muda unavyozidi kusonga mbele sasa hivi, hata mtu ukihitaji line kwa
haraka, labda upitie kwa mtu aliyekwisha ipata vinginevyo ni lazima ufanye
ufuatiliaji kwa subira ndipo uweze
kuipata.
Watu kuna kitu walichogundua katika biashara hii. Mara
zote mjasiriamali aliyekuwa makini hupendelea urahisi katika kufanya biashara,
simaanishi urahi wa bei, la, bali ni
urahisi katika uendeshaji usiokuwa na ‘longolongo’ nyingi kwa mfano, biashara
hii hata kama unamuachia majukumu msaidizi ama mfanyakazi, huumii sana kichwa
kwani hesabu zake zinajulikana na
isitoshe, miamala yote hurekodiwa kiteknolojia na kampuni husika ambapo huwa rahisi
mwisho wa mwezi au kipindi cha biashara kuja kupewa kamisheni ya miamala
iliyofanyika. Hakuibii mtu hapa.
Uzuri mwingine wa biashara hii ya uwakala wa makampuni ya
simu ni kwamba, jioni baada ya kufunga kazi mjasiriamali unafahamu mara moja
faida uliyopata katika siku husika kulingana na idadi ya watu na kiasi cha
miamala waliyofanya. Husumbuani na mteja kwenye bei kwani bei zinakuwa
zimeshapangwa tayari na makampuni, na hamna shida ya wateja kwani mahitaji ya
huduma za kipesa ni mengi na mawakala bado ni wachache nchini.
........................................................................................................
Ndugu msomaji, kampuni yako ya Self Help Books publishers ltd inatangaza rasmi kwamba vile vitabu vilivyokuwa vimekwisha sasa zimeshachapwa nakala nyingine na vinapatikana ukiwa sehemu yeyote nchini, na wale waliokuwa wametoa oda zao pia zipo tayari. Ukihitaji kitabu chochote kile tuwasiliane kwa namba zilizoko katika blogu hii au 0712 202244 au 0765 553030
asnte kwa maelezo mazuri
ReplyDeleteAsante pia ndugu Mfutakamba kwa kusoma hapa.
DeleteAsante kwa ushauri.... Me nipo chuo nataman kufanya Sana hii biashara ya Pesa za kimtandao Lakin Sina Elimu Sana na hii biashara.... Naomba msaada wa kiushaur
ReplyDelete