Watanzania wenye asili ya kisomali, hata na wengine
waishio nchini kama wakimbizi, ni nadra
sana kuwakuta wakiishi maisha magumu kiuchumi. Na si hapa Tanzania tu, bali
kote duniani walipo watu hawa wa jamii
ya Kisomali kama vile huko Ulaya Marekani na hata Asia. Licha ya nchi yao kuwa
na matatizo makubwa ya kliusalama kwa takriban zaidi ya miaka 20 sasa tangu
kupinduliwa kwa dikteta Mohamed Siad Barre kila
wanakokimbilia wengi wao huwakuta wakimiliki biashara kubwakubwa.
Baada ya kufikiria
na kuamua kufanya ‘kautafiti’ kasikokuwa rasmi nimeshangazwa na majibu
niliyokutana nayo. Kwanza nilianza kwa kuwadodosa waswahili wenzangu na wengi
wao walinipa majibu kama vile, “ Wasomali wengi shughuli zao hazieleweki, ni
wajanja sana na hata wakati mwingine hutumia njia haramu kama vile utekaji
nyara , usafirishaji na uuzaji wa sila, madawa ya kulevya pamoja na uharamia wa
baharini.” Mwingine, “Hawa watu bwana wana ushirikiano mkubwa sana, baadhi ya
ndugu huchangiana pesa kusudi mmoja au wawili waende ulaya au nchi yeyote yenye
neema, baadaye wanapokwenda kufanikiwa kiuchumi huwatumia ndugu waliobaki
nyumbani mitaji na hiyo ndiyo siri yao kuu ya mafanikio”
Kuna waliodiriki hata kusema kuwa , “Wasomali bwana
wanapofanya biashara zao huwa wana kawaida ya kuchinja wanyama kama mbuzi na
kondoo, sijui kama ni kafara ama kitu gani kwani hata kama unaishi nao jirani
hawawezi kukushirikisha. Hugawiana nyama wenyewe kwa wenyewe na wasomali
wanaofahamiana, huenda ikawa matambiko hayo ndiyo chanzo cha wao kufanikiwa
katika biashara zao”
Baada ya kupata maoni mengi toka kwa wazawa wa hapa, niliamua nitende haki kama
ilivyokuwa sheria ya maumbile kuwa usije ukamhukumu mtu kwa ushahidi wa upande
mmoja pekee. Nikaanza na wasomali fulani wanaoishi jirani na ninapofanya
shughuli zangu za kila siku.Huwa napenda kupiga nao stori mara nyingi ingawa
wengi wao hawakijui Kiswahili barabara.
Kuna mmoja dereva wa malori makubwa jina sijalishika huwa anapenda sana
kunitania, ”wewe mswahili achana na biashara yako hii ya …………….(huitaja biashara yangu)twende zetu Sudani ya Kusini
nikakuonyeshe biashara itakayokutajirisha harakaharaka” Na mimi huwa namtania
“Wewe Msomali, mimi siyo mjinga, nani wa
kwenda kujiunga na ‘Al Shabaab’? Siwezi kwenda kujifunga mabomu mie niache”
Hujaribu kunishawishi nitafune mirungi lakini huwa namwambia, “mimi siyo mbuzi,
hebu ondoka hapa wala asije akatokea polisi huko nikaingia mtego usiokuwa
wakwangu”.
Kuna kijana mwingine wa Kisomali jina lake Haruni, yeye
ni kama vile hajui Kiswahili kabisa hutamka maneno kwa shida mno, na inaonekana hapa hajakaa muda
mrefu, baba yake anamiliki malori makubwa yaendayo Congo, na huniambia kuwa
mama yake yupo Marekani na huko wanamiliki nyumba, na umri wake wapata kama
miaka 40 hivi. Mwaka jana alisafiri kwenda Marekani na baada ya miezi michache akarudi tena
hapa Tanzania akasema amekuja kumsaidia
baba yake kwenye kampuni yake ya usafirishaji mizigo.
Naye hupenda sana kunitania huku akitumia lugha ya
Kiswahili kibovukibovu
kilichochanganyikana na kiingereza. Leo alipofika akaanza kunitania,
“Wewe kila siku nikija hapa unaonekana uko ‘sirias’ , hucheki muda wote umekaa ndani umejiinamia , mimi
mwenzio umewahi kuniona nimenuna hivyo muda wote? toka nje uje ujumuike na watu, uzungumze,
pesa hazitafutwi hivyo.” Na mimi sikuchelewa nikamjibu, “ Siyo wewe
uliyeniambia siku za mwisho wa wiki ijumaa na Jumamosi hata mkeo hakusemeshi,
ni siku zako za kutafakari? Sasa huko siyo kununa ni kitu gani? Hata na mimi
nina muda sipendi kusemeshwa natafakari mambo yangu”.
Baada ya utani huo wa hapa na pale, nikajikuta namwambia,
sichangamki kutokana na ukata, sina pesa, nawaza jinsi ya kupata pesa. Baada tu
ya kutamka sentensi hiyo ndipo yakazuka mazungumzo yaliyokuja kuzaa wazo lililonisukuma kuandika makala hii. Aliniambia hivi;
“Listen, I am forty now, my son, 18 he is in USA studying at Goverment boarding school, I pay no single pen. I started Saving money when I was 14, after that I invested in business and now I am retired at 40” Akimaanisha kwamba kinachotakiwa ili mtu uishi maisha mazuri, kwanza anza mapema kujiwekea akiba, kisha itumie akiba hiyo kuwekeza katika biashara hasa hasa ni vizuri zaidi ikiwa utawekeza katika nyumba na ardhi. Utajikuta ukistaafu mapema ukiwa bado kijana wa umri wa miaka 40.
“Listen, I am forty now, my son, 18 he is in USA studying at Goverment boarding school, I pay no single pen. I started Saving money when I was 14, after that I invested in business and now I am retired at 40” Akimaanisha kwamba kinachotakiwa ili mtu uishi maisha mazuri, kwanza anza mapema kujiwekea akiba, kisha itumie akiba hiyo kuwekeza katika biashara hasa hasa ni vizuri zaidi ikiwa utawekeza katika nyumba na ardhi. Utajikuta ukistaafu mapema ukiwa bado kijana wa umri wa miaka 40.
Nilipata jibu kwa nini
Wasomali kama walivyokuwa wenzao Wayahudi kila sehemu wanapokwenda duniani hufanikiwa
kiuchumi na maisha yao hubadilika huku wenyeji walioko pale wakiendelea
kuwakodolea macho huku wakisema maneno wasiyokuwa na ushahidi nayo. Kwa
kufahamu changamoto walizokuwa nazo huko kwao, hakukaliki, hawana jingine zaidi ya kuhakikisha fursa yeyote
wanayoipata hawaichezei, hawarudii makosa, “wanaamua kuichoma meli waliyokwenda nayo pale ili wasipate tena wazo
la kurudi nyuma, ni ama wafe au washinde
vita, ‘fullstop’”
0 Response to "WASOMALI KUFANIKIWA BIASHARA NA KUTAJIRIKA: MWENZAO ATOBOA SIRI"
Post a Comment