Mfano mzuri ni jana wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akizindua rasmi Azam TV jijini Dar es salaam, nilikuta vijana fulani mahali wakiitana, mmoja akiwaambia wenzake, “njooni haraka mumuone Baresa, kwenye tv, mlisema huwa haonekani sasa huyu ni nani?
Kumbe vijana wale kuna siku walibishana nusu wapigane,
kisa eti wengine wakisema Baresa anaonekana hadharani na wengine wakibisha
kabisa na kusema, Baresa hawezi kabisa kuonekana hadharani. Ni watu wengi
waliokuwa wakimsikia Bakhresa kwa jina tu huku wakitamani japo siku moja waione
sura yake.
Nilithibitisha hilo baada ya siku moja nilipokuwa
nimeshika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA ambacho
juu ya jalada kuna picha za Mabilionea wetu watatu,kushoto, Mzee Reginald
Mengi, katikati Mzee Said Salim Bakhresa na kulia MO au Mohamed Dewj, kila
aliyekuwa akikiangalia kile kitabu aliniuliza huyu hapa katikati ni nani? Ni wachache
waliokuwa wakigundua kuwa ndiye Bakhresa.
Kitabu
“Mifereji 7 ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa”
|
Habari za uzinduzi wa Azam TV kwa kina unaweza ukazipata
zaidi katika blogu hii hapa ya Tanzania Today
0 Response to "BILIONEA BAKHRESA AZINDUA RASMI AZAM TV"
Post a Comment