inatoka sehemu ya pili
Na wewe pia waweza kujua kwamba kila kiongozi mkubwa tangu mwanzo wa ustaarabu mpaka sasa hivi
alianza na ndoto. Ikiwa hautaweza kuuona utajiri mkubwa katika fikra zako, basi
kamwe hautaweza kuuona katika balansi yako ya benki. Kamwe haijawahi kuwepo
fursa kubwa kwa waotajindoto kivitendo kama ilivyokuwa sasa.
Sisi ambao tulio katika mbio za kusaka utajiri tunapaswa
kutiwa moyo kufahamu kwamba, Dunia hii inayobadilika, ambamo tunaishi ndani
yake, inahitaji mawazo mapya, njia mpya za kutenda mambo, viongozi wapya,
ugunduzi mpya, njia mpya za kufundisha, njia mpya za kutafuta masoko, vitabu
vipya, fasihi mpya, matumizi mapya ya kompyuta, tiba mpya za maradhi na njia
mpya kwa kila nyanja ya biashara na maisha.
Nyuma ya mahitaji hayo kwa vitu vipya na vizuri zaidi
kuna sifa moja ambayo mtu ni lazima kwanza awe nayo kusudi aweze kushinda, nayo
ni, ukamilifu
wa lengo, elimu ya ni nini
mtu anachokitaka, pamoja na shauku kuu ya kukimiliki.
Ili kutimiza hilo, anatakiwa muotajindoto kivitendo
ambaye anaweza, na atakayeziweka ndoto zake katika vitendo. Waotajindoto
kivitendo daima wamekuwa, na daima watakuwa wachora kielelezo cha ustaarabu.
Sisi tuliokuwa na shauku ya kujichumia utajiri, tunapaswa kukumbuka kwamba
viongozi wa kweli wa Dunia, daima wamekuwa watu wenye kutumia, na kuweka katika
vitendo nguvu isiyoshikika wala kuonekana ya fursa ambayo bado haijazaliwa.
Wamebadilisha nguvu hizo (au msukumo wa fikra) kuwa majengo marefu, miji
mikubwa, viwanda, ndege, magari, huduma bora za afya na kila aina ya hali bora
inayofanya maisha kuwa yenye furaha.
Ustahimilifu na akili iliyofunguka ni mahitaji ya
kivitendo kwa muotajindoto wa leo. Wale ambao ni waoga wa mawazo mapya
hushindwa kabla hawajaanza. Haijawahi kutokea wakati muafaka zaidi kwa
waasisi kushinda sasa. Kuna biashara
nyingi zisizomithilika, dunia ya kifedha na kiviwanda kuumbwa tena upya na
kuelekezwa sambamba na njia mpya zilizokuwa bora zaidi.
Katika kupanga kupata mgawo wako wa utajiri, usiruhusu
mtu akushawishi kumdharau muotajindoto. Kuvishinda vigingi vikubwa katika hii
dunia inayobadilika kila wakati, ni lazima uwe na roho ya waasisi wakubwa wa
zamani ambao ndoto zao zimeupa ustaarabu kila kitu cha thamani uliyokuwa nacho,
roho ambayo hutumikia mithili ya damu ya uhai wa jamii yetu-nafasi yako na
yakwangu, kuendeleza na kutafuta soko la vipaji vyetu.
Tusisahau, Columbus aliota juu ya Dunia isiyojulikana,
akihatarisha maisha yake kwa uwepo wa dunia hiyo, na aliivumbua! Copernicus,
mwana-elimu ya anga, aliota juu ya uwepo wa sayari nyingi, na hilo
alilithibitisha! Baada ya kusherekea ushindi hakuna mtu aliyemshutumu hadharani
kuwa aliyoyasema yalikuwa hayatekelezeki. Badala yake Dunia ilitoa heshima kubwa
kwenye kaburi lake, hivyo kuthibitisha kwa mara nyingine tena kwamba, mafanikio
hayahitaji kuomba radhi, kushindwa hakuna kisingizio.
Itaendelea sehemu ya nne...........
------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------
**Usisahau, vitabu bado vipo
wahi nakala yako kabla havijamalizika.
0 Response to "MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA KISINGIZIO"
Post a Comment