Inatoka sehemu ya i kama hukuisoma isome hapa.
Asubuhi moja baada ya moto mkubwa wa Chicago, kundi la wafanyibiashara walisimama kwenye barabara ya umma, wakitazama mabaki ya moshi wa yaliyokuwa maduka yao. Walifanya mkutano kuamua ikiwa kama wangejaribu kujenga tena upya, au kuhama Chicago na kwenda kuanza tena katika eneo jingine la nchi ambalo lingekuwa na matumaini zaidi.Wote isipokuwa mmoja wao, walifikia uamuzi wa kuondoka Chicago.
Mfanyabiashara aliyeamua kubaki na kujenga upya,
alinyosha kidole kwenye mabaki ya lile duka lake, na kusema, “Mabwana, juu ya
eneo lilelile nitajenga duka kubwa kuliko yote Duniani, pasipokujali ni mara
ngapi litaungua”. Duka lilijengwa, na mpaka leo hii lipo jengo refu la
ukumbusho kwa nguvu ya ile hali ya akili iitwayo Shauku kuu.
Kitu rahisi kwa jemadari mkuu kufanya kingeweza kuwa
sawasawa na kile wafanyabiashara wenzake walichofanya. Safari ilipokuwa ngumu
na majaaliwa ya baadae kuonekana ni yenye majonzi, walisita na kuelekea kule
walikoona mambo ni rahisi.
Kumbuka vyema tofauti hii kati ya Jemadari na
Wafanyabiashara wenzake, kwasababu ni tofauti hiyohiyo inayomtofautisha Edwin
C. Barnes na maelfu ya vijana wengine waliowahi kufanya kazi katika kampuni ya
Edison. Ni tofauti hiyohiyo ambayo hutofautisha kivitendo wale wote
wanaofanikiwa na wale wanaofeli.
Kila binadamu anayefahamu makusudi ya pesa, hutamani
kuzipata. Kutamani peke yake hakutaleta utajiri. Lakini kutamani utajiri huku
ukiwa na hali ya akili iliyokuwa na utayari, kisha ukapanga mipango dhahiri na njia
za kuufikia utajiri, na ukaisaidia hiyo mipango kwa uvumilivu usiotambua
anguko(kufeli) kutaleta utajiri.
Njia ambayo shauku ya utajiri inaweza kubadilishwa na
kugeuka kuwa katika kipimo cha pesa imegawanyika katika hatua sita kamili za
kivitendo,
1. Jenga picha akilini mwako ya kiasi kamili cha
pesa unachotamani, haitoshi tu kusema, “Nataka kiasi kikubwa cha pesa”, kuwa
muwazi ni kiasi gani (Kuna sababu za kisaikolojia kutaja kiasi kamili, ambazo
zitaelezwa katika sura inayofuata.
2. Tambua hasa ni kitu gani unachokusudia
kurudisha kama malipo kwa fedha unazotamani(Ukweli
ni kwamba, hakuna kitu cha bure)
3. Weka tarehe kamili ni lini unakusudia
kumiliki pesa unazotamani.
4. Tengeneza mpango kamili wa kutekeleza tamanio
lako, na anza mara moja pasipo kujali kama upo tayari kuuweka mpango huo katika
vitendo ama la.
5. Andika sentensi fupi na inayoeleweka ya kiasi
cha pesa unachokusudia kupata. Taja muda wa mwisho wa kuzipata. Eleza kile
unachokusudia kutoa kama malipo kwa pesa utakazopata, na elezea kwa ufasaha
mpango ambao kwa kupitia huo umekusudia kuzikusanya.
6. Soma sentensi yako uliyoandika kwa sauti mara
mbili kwa siku, mara moja punde kabla hujalala usiku, na mara moja baada ya
kuamka asubuhi. WAKATI UKISOMA, ONA NA HISI NA AMINI WEWE MWENYEWE TAYARI UKIWA
UNAMILIKI HIZO PESA.
Ni muhimu kwamba unafuata maelezo yaliyoelezwa katika
hizi hatua sita. Ni muhimu zaidi kwamba unazingatia na kufuata maelekezo katika
aya ya sita .
Unaweza ukalalamika kwamba, haiwezekani kwa wewe, “kuona
mwenyewe ukimiliki pesa kabla hujawa nazo kiukweli. Hapa ndipo shauku kuu
inapoanza kufanya kazi. Ikiwa kweli unatamani sana pesa kiasi ambacho tamaa
yako umeijaza akilini, hautapata ugumu katika kujishawishi mwenyewe kwamba
utazipata.
Ni wale tu wenye utambuzi wa pesa wanaoweza kulimbikiza
utajiri mkubwa. Utambuzi wa pesa maana yake ni kwamba akili imejawa mno na hamu
ya pesa kiasi kwamba mtu anaweza kujihisi mwenyewe kuwa tayari anazimiliki.
Kwa wale ambao hawajapata elimu ya jinsi akili ya
binadamu inavyofanya kazi, maelekezo haya yanaweza yakawa hayatekelezeki
kivitendo. Yanaweza yakawa msaada, kwa wale wote wanaoshindwa kutambua mantiki
ya zile hatua sita, kujua kwamba taarifa wanazopata zilitoka kwa Andrew
Carnegie ambaye alianza kama kibarua wa kawaida tu kwenye kiwanda cha chuma.
Licha ya mwanzo wake duni Carnegie aliweza kuzifanya
kanuni hizi kumpatia utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya dolla million 100.
Yaweza kuwa msaada zaidi kujua kwamba hatua sita zilizopendekezwa hapa zilichunguzwa
kwa makini na Thomas A. Edison.
Aligonga mhuri wa kibali juu yake kuashiria siyo tu
kwamba hatua hizo ni kwa ajili ya kujichumia pesa peke yake, bali pia ni kwa
ajili ya kulifikia lengo lolote lililokuwa dhahiri. Hatua hizo hazihitaji “kufanya
kazi ngumu” Hazihitaji kujitoa mhanga. Hazihitaji mtu kuwa na dharau, au kuwa
mjinga. Ili kuzitumia hauhitaji kuwa na kiwango kikubwa cha elimu.
Lakini matumizi yenye tija ya hizi hatua sita yanahitaji
ubunifu wa kutosha kumuwezesha mtu kuona na kuelewa, kwamba utajiri hauwezi
ukatokea tu kwa bahati na sibu. Mtu anapaswa kutambua yakwamba, wale wote ambao wamewahi kujilimbikizia
utajiri mkubwa, kitu cha kwanza kabisa kufanya kabla hawajapata pesa, kwa kiasi
fulani waliota ndoto, kuwa na matumaini, kuwa na matamanio, shauku na mipango.
---------------------------------------------------------------------------------------
Usikose sehemu
ya (iii) kesho,tutaendelea kuwa pamoja na tunakutakia safari njema kuelekea
mafanikio katika shughuli zako.
Ngugu msomaji kama kuna chochote ambacho ungependa tuboreshe katika blogu hii au una maoni yeyote tafadhali yaweke hapo chini sehemu ya kutoa maoni na si lazima ujitambulishe. Pia tunapenda kuwajulisha kwamba vitabu vyote vya Self Help Books, "Mifereji ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa", "Siri ya mafanikio Biashara ya rejareja" na "Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali", sasa vyote vimekamilika.
Ukiwa Dar es salaam unaweza kuvipata kwa mawakala wetu au katika duka lililopo nje ya ofisi zetu Buguruni sokoni stendi mbele kidogo ya Benki ya Akiba simu zetu ni '0712 202244'/ '0765 553030'. Na kama uko mikoani, mkoa wowote ule tutakutumia kwa njia ya Mabasi au unaweza ukamuagizia mtu/jamaa yako anayefika Dar akuchukulie.
0 Response to "WEKA TAREHE KAMILI NI LINI UNAKUSUDIA KUMILIKI PESA UNAZOTAMANI"
Post a Comment